JESHI LA KUJENGA TAIFA LITAANDIKISHA VIJANA WA KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA KUANZIA JANUARI 2014. NAFASI HIZO ZIMETOLEWA KWA TANZANIA BARA NA VISIWANI.
USAILI UTAANZIA NGAZI ZA WILAYA HADI MIKOA. VIJANA WANAOPENDA KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI WAPELEKE MAOMBI YAO KWENYE WILAYA WALIKO.
MAFUNZO YATAANZA MWEZI MACHI KWA WATAKAOCHAGULIWA.
SIFA NA MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Awe raia wa Tanzania.
2. Awe na umri wa miaka 18 hadi 23.
3. Awe na elimu ya darasa la saba hadi kidato cha sita.
4. Asiwe ameoa, kuolewa na asiwe na mtu anayemtegemea.
5. Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa.
6. Awe na tabia na mwenendo mzuri.
7. Awe tayari kufuata sheria zote za Kijeshi zitakazokuwa juu yake wakati akiwa Jeshini (kutoroka, wizi, ulevi, uvutaji bangi, madawa ya kulevya , upatikanaji wa mimba n,k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushitakiwa na kusitishiwa mkatba waako na Jeshi la Kujenga Taifa.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA JKT , JAN , 2014
Reviewed by Unknown
on
3:08:00 AM
Rating: