AFISA UTALII DARAJA LA II– NAFASI 1

Afisa Utalii Daraja La Ii – Nafasi 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.
13.1 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu katika fani ya Utalii kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
13.2 MSHAHARA • Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
13.3 MAJUKUMU YA KAZI
• Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
wadau wote.
• Kutoa Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii.
• Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii.
• Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi.
• Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii.
• Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii.
• Kuandaa kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii.
• Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli.
• Kukagua hoteli, loji na migahawa.
• Kujibu na kufatilia malalamiko yanayoletwa na watalii.
• Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakala wa utalii.
• Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na Washika dau wote.
• Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia/kutoa wageni.
• Kutunza kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii.
• Kutayarisha taarifa ya kila mwezi ya takwimu za watalii waliongia nchini na mapato yaliyopatikana.
• Kufanya tafiti ngo “Survey” kwenye Hifadhi za Taifa na maeneo tengefu ili kupata idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii.
• Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini.
• Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii.
• Kutayarisha ripoti za mwezi, robo mwaka, na za mwaka mzima.
• Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya suervey.
• Kuitisha mikutano ya Tourism Facilitation Committee.
• Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kukufuatilia utekelezaji wa maazimio.
• Kupitia miongozo inayohusu “Tourism Facilitation Committee”.
• Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii.
• Kutayarisha kuhakiki vivutio vya utalii nchini.
• Kuitisha mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii.
• Kushiriki katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii.
• Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimali za mazingira katika shughuli zihusuzo utalii na mazingira.
• Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 877 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. -Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI -Computer Certificate -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) -Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 Julai, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
 


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma
S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM.
AFISA UTALII DARAJA LA II– NAFASI 1 AFISA UTALII DARAJA LA II– NAFASI 1 Reviewed by Unknown on 7:53:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.