Kumb. Na EA.7/96/01/E/27 30 Desemba, 2013
TANGAZO LA NAFASI ZA
KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi 115 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe
katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja
na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
“Transcripts”, “Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji
wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 13 Januari,
2013
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA).
xv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
1.0
DEREVA MASHUA/VIVUKO DARAJA LA II (FERRY/
BOAT OPERATOR GRADE II) - NAFASI 3
Nafasi hii ni kwa ajili ya Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA)
·
Kufunga
na kufungua kamba za mashua/kivuko.
·
Kuchunga
usalama nwa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko.
·
Kupanga
abiria au magari kwenye mashua/kivuko.
·
Kuendesha
na kuongoza mashua/kivuko.
·
Kutunza
daftari za safari ya mashua/kivuko.
·
Kuhakikisha
kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
·
Kuangalia
mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha
IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo
cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na
Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita
ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye
mashua/vivuko.
1.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi
2.0
AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS
OFFICER GRADE II) – NAFASI 3
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu,
Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
Hili
ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Maafisa
Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile
zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la I:-
·
Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na
kusimamia matumizi ya kumbukumbu.
·
Kutambua
na kutafuta kumbukumbu katika masjala.
·
Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa
na kompyuta, kutunza na kusimamia matumizi yake.
·
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Kwanza katika
fani ya Utawala,Kumbukumbu na Nyaraka kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa
na Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
3.1
MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 15
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kupokea
wageni na kuwasaili shida zao.
·
Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya
uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa
kupokea wageni.
·
Kupokea
na kusambaza maombi ya simu za ndani.
·
Kutunza
na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
·
Kuwaelekeza
wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
·
Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani
wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.
·
Kupokea
simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
·
Kupokea
simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
·
Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka
nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
3.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wahitimu
wa Kidato cha
IV waliofaulu masomo
ya Kiingereza,
|
|
Kiswahili na Hisabati na kufuzu
mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu
|
|
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.
|
3.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
4.1
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL
SECRETARY GRADE III) – NAFASI 30
4.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuchapa
barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
·
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida
zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
·
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za
matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi
zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
·
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake
majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo
ofisini.
4
·
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa
kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa
amepewa na wasaidizi hao.
·
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa
Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
·
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa
na Msimamizi wake wa kazi.
4.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV
waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe
wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika
moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa
na Serikali na kupata cheti katika programu za Window, Microstoft Office,
Internet, E-mail na Publisher.
4.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
5.1
MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 15
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi
inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
·
Kuhahikisha
kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
·
Kulinda
usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
·
Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote
yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
·
Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia
katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
·
Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea
katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika.
·
Kutoa
ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne
waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
|
|
·
|
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
|
5.4
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
6.1
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (NYARAKA) DARAJA LA II – (RECORDS
MANAGEMENT ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 25
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo
atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi
atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja
I:-
·
Kutafuta
kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
·
Kudhibiti
upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
·
Kuchambua, kuorodhesha na kupanga
kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and
boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
·
Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki
(file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
·
Kuweka
kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
·
Kushughulikia
maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne (IV) au sita (VI)
wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika fani ya Masjala.
6.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi.
7.0
MSAIDIZI WA OFISI – NAFASI 22
7.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na
ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani,
kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha
vyoo.
·
Kuchukua na kupeleka majalada na hati
nyingine kwsa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·
Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi
atakavyoelekezwa.
·
Kutayarisha chai ya ofisi.
·
Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua
kutoka Posta.
· Kuhakikisha kwamba
vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinastahili.
·
Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati
wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
·
Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine
za kudurufia.
·
Kuweka katika majalada nakala za barua
zilizochapwa katika ofisi walizomo.
·
Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila
vinapoharibika.
7.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri
katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
7.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
8.0 MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER
ENGINEER GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Tawala Mkoa wa Geita,
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Ujenzi na Usimamizi wa Vituo vya Hali ya
Hewa, Vituo vya Upimaji wingi wa Maji mitoni (Discharge Measurements) na
Uchukuaji wa sampuli za mchanga unaosafirishwa kwenye mito (sedment sampling)
na kuzitafsiri.
·
Ukusanyaji wa takwimu kwenye vituo vya hali
ya hewa na upimaji wa wingi wa maji mitoni na kuzitafsri takwimu hizo.
·
Kuandaa na kutayarisha Taarifa ya robo, nusu
na mwaka mzima katika sehemu ya Haidrologia.
·
Kutayarisha
kielelezo cha mtiririko wa maji ( Rating Curve Eqution )
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa
Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na
ujuzi wa kutumia kompyuta.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za
mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
X. M. DAUDI
SECRETARY
JOBS IN TANZANIA JAN 2014
Reviewed by Unknown
on
1:14:00 AM
Rating: