TANGAZO LA KAZI
1.0 NAFASI YA MHARIRI WA VIDEO NA PICHA
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kinawatangazia Watanzania wote hususan Wanachama nafasi ya kazi ya Mhariri wa Video na Picha Mnato (Video Editor) ili kujaza nafasi wazi Makao Makuu ya Chama.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
- Ø Kupiga Picha mnato na video kwenye shughuli mbalimbali za Chama.(Shooting)
- Ø Kuhariri Picha kwa kushirikiana na Idara zinazohusika ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa (Editing)
- Ø Kutengeneza CD na DVD za shughuli mbalimbali za Chama. (Production)
- Ø Kutengeneza Clips ndogo ndogo kwa ajili ya ChademaTV.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
- Ø Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 3
- Ø Elimu ngazi ya Stashahada kwenye chuo kinachotambulika na Serikali
- Ø Awa na Afya njema itakayomwezesha kusafiri sehemu mbalimbali nchini kwa muda mrefu.
- Ø Uandishi wa Habari ni Sifa ya Ziada ya Faida.
- Ø Umri usizidi miaka 35
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Viwango vya Chama yaani CDM 3 Kwa viwango vya CHADEMA
1.4 MAELEZO YA JUMLA
Mwisho wa maombi ni tarehe 20 July 2014. Waombaji wachache waliofanikiwa wataitwa kwa ajili ya Usaili.
Maombi yatumwe kwa baruapepe info@chadema.or.tz
Au kwa Anuani ifuatayo;
Katibu Mkuu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
P.O.Box 31191
Dar es Salaam
NB:
Maombi yaambatane na Clip isiyozidi muda wa dakika mbili (2) yenye ujumbe kwa jamii inayoonyesha kazi iliyofanywa na Muombaji kama Attachment kwenye baruapepe au kwa njia ya CD kwa maombi kwa njia ya Posta.
MHARIRI WA VIDEO NA PICHA
Reviewed by Unknown
on
11:51:00 PM
Rating: