MAJUKUMU NA WAJIBU WA AFISA ULINZI WA WANYAMAPORI
1. Atakuwa kiongozi Askari jamii wa wanyamapori wa Jumuiya.
2. Kuandaa mpango kazi wa ulinzi wa Jumuiya na kusimamia utekelezaji wake.
3. Kuweza kutoa mafunzo ya mbinu za kupambana na ujangili kwa askari jamii wa wanyamapori ndani ya Jumuiya.
4. Kuandaa taarifa zote za ulinzi na usalama na taarifa za kambi za askari jamii wa wanyapori.
5. Kufanya kazi zote kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA:
1. Awe na stashahada kutoka chuo cha usimamizi wa wanyamapori Mweka au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali au Awe alishawahi kuwa Afisa katika jeshi la Polisi, Jeshi la wananchi, TANAPA au Idara ya Wanyamapori.
2. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitano (5) katika mambo ya ulinzi usalama au ulinzi dhidi ya ujangili.
3. Awe hajaukumiwa kwa makosa yoyote ya jinai.
4. Awe na umri chini ya miaka arobaini na tano(45)
Barua zote ziandikwe kwa:-
Katibu,
Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori Burunge,
S.L.P. 104,
BABATI.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti. Siku ya usahili waombaji wote waje na vyeti halisi (original).
• Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30.07.2014, saa 9:00 alasiri.
AFISA ULINZI WA WANYAMAPORI
Reviewed by Unknown
on
4:39:00 AM
Rating: