9.0
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
(NYARAKA) – NAFASI 50
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo
atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi
atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja
la I
·
Kutafuta
kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
·
Kudhibiti
upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
·
Kuchambua, kuorodhesha na kupanga
kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and
boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
·
Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki
(file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
·
Kuweka
kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
·
Kushughulikia
maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha sita wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya,
Masjala, Mahakama na Ardhi.
9.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS B kwa mwezi
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe19 Agosti, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
Public Service Recruitment
| |
Utumishi wa Umma,
|
Secretariat,
| |
SLP.63100,
|
P.O.Box 63100
| |
Dar es Salaam.
|
Dar es Salaam.
|
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NYARAKA) – NAFASI 50
Reviewed by Unknown
on
12:26:00 PM
Rating: