OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb.
Na EA.7/96/01/G/55 26
Agosti, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA
KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje
na Ushirikiano wa Kimataifa.
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa
zinazohusu masuala ya kimahusiano ya kimataifa.
·
Kuhudhuria
mikutano mbalimbali.
·
Kuandaa
mahojiano.
·
Kufuatilia
masuala mbalimbali ya kimataifa.
·
Kufanya
utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
·
Kutunza
kumbukumbu za matukio mbalimbali.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao
wamejiimarisha (major) katika fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations),
Sheria au Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha, wawe wamefanya na kufaulu mtihani
unaotolewa Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.
1.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL
SECRETARY GRADE III) – NAFASI 11
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuchapa
barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
·
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida
zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
·
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za
matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi
zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
·
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake
majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo
ofisini.
·
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa
kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa
amepewa na wasaidizi hao.
·
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa
Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
·
Kutekeleza
kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
|
|
·
|
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
|
|
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na
|
|
Kiingereza maneno
80 kwa dakika
moja na wawe
wamepata mafunzo ya
|
|
Kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
|
|
katika programu za Window,
Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
|
2.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
3.1
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN
RESOURCES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote
katika Wizara, Mikoa, Wilaya na Idara zinazojitegemea kulingana na mahali
alipo.
·
Kutafsiri
na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
·
Kutafiti,
kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
·
Kuandaa
na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
·
Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya
mafunzo kwa kushirikiana na vyuo vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
·
Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na
kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
3.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi
Jamii au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
§ Menejimenti
ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
§ Elimu
ya Jamii (Sociologly).
§ Utawala
na Uongozi (Public Administration).
·
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
3.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
4.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kupokea
wageni na kuwasaili shida zao.
·
Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya
uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa
kupokea wageni.
·
Kupokea
na kusambaza maombi ya simu za ndani.
·
Kutunza
na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
·
Kuwaelekeza
wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
·
Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani
wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.
·
Kupokea
simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
·
Kupokea
simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
·
Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka
nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
4.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV
waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
|
|
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya
Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
|
|
vinavyotambuliwa na Serikali.
|
4.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
5.1
MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na
ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani,
kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha
vyoo.
·
Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine
kwa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·
Kusambaza
barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
·
Kutayarisha
chai ya ofisi.
·
Kupeleka
mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
·
Kuhakikisha
kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
·
Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati
wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
·
Kuweka
katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
·
Kutunza
vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
5.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wahitimu
wa kidato cha
nne waliofaulu vizuri
katika masomo ya
|
|
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
|
5.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
na wenye umri usiozidi miaka 45
i.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iii.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo,
nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa
sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
x.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September,
2014
xii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MAMBO YA NJE - 26 Agosti, 2014
Reviewed by Unknown
on
12:25:00 PM
Rating: