(A) SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe na Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV
2. Awe na Leseni daraja la “C” ya uendeshaji, uelewa mzuri wa alama za barabarani pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitano (5) bila kusababisha ajali
3. Awe na Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II
4. Awe na nidhamu, uaminifu na mtiifu
5. Awe ni mtunza siri za ofisi
6. Awe na uzoefu wa shughuli za “Clearing & Forwarding”
(B) MAJUKUMU YA KAZI
1. Kuendesha magari ya Bodi kama atakavyopangiwa na Mkuu wake wa Kazi
2. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote
3. kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo na kuhakikisha gari linakwenda “service” kila inapohitajika
4. Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
5. Kutoa taarifa mara moja kuhusu hitilafu/ matatizo ya gari
6. Kumhudumia kwa heshima afisa atakayepangiwa kumuendesha
7. Kuhakikisha leseni ya gari na Bima ni hai wakati wote
8. Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote
9. Kutekeleza kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wa Kazi
1
(C) MSHAHARA
Mshahara wa kuvutia utatolewa kwa mwombaji atakayefanikiwa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.
1. Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania.
2. Barua zote ziambatanishwe na vivuli vya vyeti husika vya kuzaliwa, matokeo ya Sekondari na Vyuo pamoja na sifa za ziada.
3. Barua zote ziwe na anwani ya uhakika na namba za simu za kuaminika
4. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 31 Octoba, 2011
Maombi yaandikwe kwa mkono (hand written) kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia anuani ifuatayo.
Meneja wa Tawi,
Bodi ya Kahawa Tanzania,
Tawi la Tanga,
S.L.P 5046,
TANGA.
AU
Branch Manager,
Tanzania Coffee Board,
Tanga Branch,
P.O. Box 5046,
TANGA.
NAFASI YA KAZI - DEREVA
Reviewed by Unknown
on
1:21:00 AM
Rating:
No comments: