MJIOLOJIA DARAJA LA
II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 8
Nafasi
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kupokea na kufuatilia upatikanaji wa taarifa
za utafiti wa mistari ya uchungi na mitetemo katika utafutaji wa madini au
petroli;
·
Kukusanya na kuchambua taarifa za mitetemo,
mienendo na mabadiliko ya miamba ardhini;
·
Kutunza
kumbukumbu za miamba, madini au petroli;
·
Kutayarisha
rasimu za taarifa za kitaalam na kuziwasilisha kunakohusika;
·
Anaweza kuongoza timu ya mafundi sanifu
wanapokuwa katika shughuli za utafutaji wa madini au petroli.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika
fani ya Jiolojia (pamoja na fani za Jiofizikia au Jiokemia) au sifa nyingine
zinazolingana na hizo kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali,
1.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani
na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo,
nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo
vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
- Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV
AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe19 Agosti,
2014
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
MJIOLOJIA DARAJA LA II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 8
Reviewed by Unknown
on
12:18:00 PM
Rating: