Loading...

Call for Interview - KUITWA KWENYE USAILI - JUNE 3 2016

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Tanzania Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The
Local Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And
Trusteeship Agency (RITA) anatarajia kuendesha Usaili na hatimaye
kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1.Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na
tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.

2.Wasailiwa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano:
kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, au hati ya kusafiria.

3.W a s a i l i w a k ufika na Vyeti Halisi vya kuanzia kidato cha IV, VI,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.

4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

5.Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

6.Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyia usaili.

7.Kila msailiwa anahitajika kufika na cheti halisi cha kuzaliwa

8.Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA)

9.Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za
kazi zitakapotangazwa

CALL FOR INTERVIEW 
Newer Posts Older Posts
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

LIKE US ON FACEBOOK

© Copyright KaziBongo | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top