Kumb. Na EA.7/96/01/H/18 13 Novemba, 2014
1.0
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 5
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
•
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
•
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki
na kila mwezi,
•
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao
katika masoko kila wiki/kila mwezi,
•
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
•
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya
pembejeo na zana,
•
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya
biashara,
•
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya
udongo na maji,
•
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa
wadau,
•
Kuandaa/kuandika
taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
•
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu
bora,
•
Kuandaa,
kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
•
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
•
Kufanya
ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya
kupitishwa,
•
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga,
matunda, maua na viungo,
•
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
• Kufanya utafiti mdogo
mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
•
Kufanya utafiti wa udongo,
•
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya
wakulima/wamwagiliaji,
•
Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa
na watafiti,
• Kuendesha/kusimamaia
vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya
mbegu.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
•
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa
kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
1.3
MSHAHARA
• Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 27 Novemba, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 5
Reviewed by Unknown
on
10:20:00 PM
Rating: