Maelezo ya Jumla
Dayosisi ya Mashariki na Pwani ni moja ya Dayosisi 24 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Dayosisi ipo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar (Pemba na Unjuja).
Wajibu wa Katibu Mkuu
Majukumu ya Katibu Mkuu yameorodheshwa kwenye Kanuni ya Dayosisi (2012) ambayo ni pamoja na kuwa Mtendaji Mkuu wa mambo yote ya utawala katika Dayosisi; Kusimamia uandaaji, uandishi na usambazaji wa mihutasari ya Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu, na Halmashauri ya Utendaji kwa kufuata taratibu; kuongoza watumishi wengine; kuwa mbunifu na mfano mzuri wa kuigwa; kuwa kiungo cha mawasiliano baina ya wadau na Ofisi Kuu ya Dayosisi; kuhakikisha kuwa Dayosisi inapata maendeleo ya kiimani, kiuchumi na kijamii; kutunza maandishi, hati muhimu, mihuri ya Dayosisi (Seal) na kumbukumbu za Dayosisi; Kutekeleza mapatano ya Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Halmashauri ya Utendaji; Kuhudhuria vikao vya Halmashauri; Kutunza na kutangaza takwimu zote za Dayosisi kadri itakavyohitajika; Kuwa mmojawapo wa wadhamini wa mali na rasilimali za Dayosisi; Kuwakilisha Dayosisi katika vikao ndani na nje ya Dayosisi; Kusimamia mapato na matumizi ya fedha na mali zote za Dayosisi; Kupokea na kutekeleza wajibu wowote mwingine kadri atakavyoagizwa na Askofu.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji awe ni Mkristo Mlutheri mwenye wito na mwenye umri usiopungua miaka 40; Awe na elimu yenye kiwango kisichopungua Shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu kinachotambulika na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) katika fani za Sheria, Uchumi, Sayansi ya Jamii, Theolojia au masuala ya Utawala/Uongozi ikifuatiwa na uzoefu kazini usiopungua miaka mitano (5) katika nafasi ya utawala; na awe mwadilifu na mwaminifu.
Aina ya Mkataba wa Ajira
Atakayefanikiwa kupata nafasi hii atapewa mkataba wa miaka minne ambayo itaweza kuongezwa kwa kipindi kingine cha pili na cha mwisho cha miaka minne.
Mshahara na Marupurupu
Mshahara na marupurupu mazuri kwa atakayefanikiwa yatalipwa kwa msingi wa maelewano.
Utaratibu wa kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe na juu ya bahasha yaandikwe:
Mwenyekiti
Kamati ya kumtafuta Katibu Mkuu
KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani
P.O. Box 837,
Dar es Salaam.

NAFASI YA KAZI YA KATIBU MKUU WA DAYOSISI
Reviewed by Unknown
on
6:51:00 AM
Rating: