Je wewe ni mjasiriamali?
Ungependa kukuza biashara yako?
BRAC Maendeleo Tanzania kupitia mradi wa Kuwezesha Kimaisha kupitia Maendeleo ya Kilimo na Mifugo (LEAD) - Mfuko wa uwekezaji ambao ni fedha maalumu kwa ajili ya kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani wa kuku na mahindi nchini Tanzania. Fedha hizi zimegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni ruzuku na mkopo. Mjasiriliamali anaweza kuomba mtaji hadi shilingi 50,000,000 kwa ajili ya uwekezaji katika biashara yako.
Kufuzu lazima biashara yako ihusiane na sekta ya ufugaji kuku na kilimo cha mahindi na pia ijiendeshe kifaida.
Kama ni msindikaji wa chakula cha kuku, mzalisha vifaranga, msindikaji wa nyama, mzalishaji wa mbegu za mahindi, msindikaji wa mahindi, n.k Unakaribishwa kutuma mombi YAKO!
Kupitia huu mfuko, tutasaidia biashara zilizopo mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Manyara, Morogoro, Tanga, Iringa, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, na Singida. Pia ilenge kuboresha uzalishaji kwa wakulima na wafugaji kuku maskini katika maeneo husika.
Unaweza kutembelea tawi la BRAC lilo karibu nawe au tembelea tovuti yetu tanzania.brac.net au barua pepe leadtzf@gmail.com kwa ajili ya kutuma maombi na maelezo zaidi kuhusu mfuko wa uwekezaji mradi wa LEAD.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Peter Munisi, Simu: 0754413533; Nelson Burton, Simu: 0758907941; Joseph Mabula, Simu: 0759247569; Shabani Isimbula, Simu: 0758838224.
Kufunga tarehe ya awamu hii ya maombi ni Febuari 8, 2016.
Download Kiswahili application form here.
FURSA ZA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI
Reviewed by Unknown
on
3:09:00 AM
Rating: