Kumb. Na
EA.7/96/01/G/24 27 Juni, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 877
za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer
Certificate
- Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA).
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 Julai,
2014
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public Service
Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
1.0
MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO –
ENGINEERS) – NAFASI 17
1.1
MAJUKUMU YA KAZI.
·
Kuandaa
program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
·
Kushiriki
katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
·
Kushiriki
kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
·
Kushiriki
katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
· Kushirikiana
na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
·
Kukusanya
takwimu za miradi ya umwagiliaji,
· Kushiriki
kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na
matumizi ya maji,
·
Kuandaa
mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
· Kufuatilia
program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya
matumizi ya wanyama na matrekta,
·
Kuwafundisha
wakulima ujenzi wa vihengo bora na
· Kushughulikia
ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
Serikali.
1.3 MSHAHARA
· Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
2.1
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO –
OFFICERS) – NAFASI 14
Nafasi
hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge, Mkurugenzi Mtendaji Halamashauri ya Wilaya ya Liwale, Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuthibiti
visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kukusanya
takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
·
Kukusanya
takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
·
Kuendesha
mafunzo ya wataalam wa kilimo,
·
Kufanya
ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
·
Ufuatiliaji
wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
·
Kuendesha
mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
·
Kutoa
habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
·
Kuandaa/kuandika
taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
·
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji
mboga, matunda, maua na mazao mengine,
·
Kusimamia/kuendeleza
uzalishaji wa mbegu bora,
·
Kuandaa,
kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
·
Kufanya
majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
· Kufanya
ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya
kupitishwa,
·
Kuendesha
mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
·
Kuhamasisha
uzalishaji wa mazao ya bustani,
· Kufanya
utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha
umwagiliaji,
·
Kufanya
utafiti wa udongo,
·
Kuhamasisha
uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
·
Kuzalisha
mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
· Kuendesha/kusimamaia
vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya
mbegu.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika
mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
· Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
3.1
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II
(AQUACULTURE) – NAFASI 3
Nafasi
hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
3.1 KAZI NA MAJUKUMU
·
Kusoma
na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha
kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
·
Kuandaana
kufundisha kozi za Wakulima.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practical).
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
3.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya AQUACULTURE
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology).
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
4.0 AFISA
KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)
– NAFASI 131
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa.
4.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushirikiana
na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,
·
Kukusanya/kuhifadhi
takwimu za majaribio,
·
Kuwafundisha
wakulima mbinu za kilimo bora,
·
Kuwafikishia
wakulima matokeo ya utafiti,
·
Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo,
matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei
kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri,
·
Kukusanya
takwimu za mvua,
·
Kushiriki
katika savei za kilimo,
·
Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu
matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,
·
Kupanga
mipango ya uzalishaji,
·
Kupima
uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
·
Kuwatambua
wasambazaji wa pembejeo,
·
Kutoa
mafunzo ya lishe kwa wakulima,
·
Kufanya
vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
·
Kudhibiti
visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kusimamia
shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
·
Kuwaelimisha
wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
·
Kutoa
ushauri wa kilimo mseto,
·
Kuandaa
sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
·
Kutoa
taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
4.2
SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3
MSHAHARA
· Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.
4.4
DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY OFFICERS) –
NAFASI 14
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mkurugenzi wa Jiji Halmashauri ya Jiji la Tanga,
Mkurugenzi wa Mji Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Katibu Tawala Mkoa wa
Dodoma, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Nyangw’ale, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge.
4.5
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa
huduma za afya ya mifugo
·
Kufanya
uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo au sehemu alipo.
·
Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia,
kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
·
Kushiriki
katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.
4.6
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree)
ya Tiba ya Mifugo
kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
4.7
MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS E kwa mwezi.
5.0
DAKTARI UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II
(VETERINARY RESEARCH OFFICER II)
–
NAFASI 7
Nafasi
hizi ni Kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kujifunza
na kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa afya na maradhi ya mifugo
·
Kuweka
kumbukumbu za utafiti
·
Kusaidia
kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
·
Kuandaa mapendekezo ya utafiti (“research
proposal”) kwa kushirikiana na Daktari Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·
Kufanya
utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
·
Kukusanya
na kuchambua takwimu za utafiti unaoendelea.
·
Kuchapisha
taarifa na makala za utafiti
·
Kuendesha
semina na maonyesho ya ufugaji bora.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree)
katika fani ya Sayansi
ya Tiba ya Mifugo (“Veterinary Science)
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali TGS E kwa mwezi.
6.0 DAKTARI MIFUGO MKUFUNZI
DARAJA LA II (VETERINARY TUTOR II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutafsiri
mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
·
Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan)
kwa upande wa nadharia na vitendo
·
Kufundisha kozi za stashahada na astashahada
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na madaktari /maofisa mifugo wa wilaya, wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practicals).
·
Kufanya
kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya
kwanza ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au
chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya
Madaktari Tanzania.
6.3 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
7.1
MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (ANIMAL
SCIENCE) – NAFASI 3
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutafsiri
mihutasari ya mafunzo kwenye masomo.
·
Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson Plan)
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha kozi za stashahada na astashahada
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendelo ya wanachuo kwa kushirikiana
na maofisa mifugo wa wilaya, viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo.
·
Kufanya kazinyingine zozote za fani yake
atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi.
8.0
AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK
OFFICER II) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Msajili Bodi ya Nyama Tanzania,
Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya
ya Sikonge.
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Atabuni
mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
·
Ataratibu
uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
·
Atasaidia
kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
·
Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji
bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
·
Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya
masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
·
Atabuni,
kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
·
Atafanya soroveya ya rasilimali (resource
survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la
kazi.
·
Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na
wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
·
Atatafiti
maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
·
Atafanya
utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
·
Atashiriki katika shughuli za kudhibiti
milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
·
Ataandaa
taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
·
Atafuatilia,
kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
·
Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani
yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
8.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo
(Animal
Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana
nayo.
8.3 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
9.1
AFISA UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II
(LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 8
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kujifunza
kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa mifugo/ndorobo
·
Kufanya
utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
·
Kuandika
na Kuweka kumbukumbu za utafiti.
·
Kusaidia
kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
·
Kuandaa mapendekezo ya utafiti (Research
Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayesimamia.
·
Kufanya
kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
9.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
9.3 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
10.0
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN
RESOURCES OFFICER GRADE II)
–
NAFASI 101
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara, Mikoa na
Halmashauri za Wilaya.
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote
katika Wizara, Mikoa, Wilaya na Idara zinazojitegemea kulingana na mahali
alipo.
·
Kutafsiri
na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
·
Kutafiti,
kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
·
Kuandaa
na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
·
Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya
mafunzo kwa kushirikiana na vyuo vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
·
Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na
kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi
Jamii au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
·
Menejimenti
ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
·
Elimu
ya Jamii (Sociologly).
·
Utawala
na Uongozi (Public Administration).
·
Mipango
ya Watumishi (Manpower Planning).
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta
10.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa
mwezi.
11.0 AFISA ARDHI MSAIDIZI –
NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Iringa.
11.1
SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato
cha Nne au Kidato cha Sita, waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya Umiliki Ardhi
na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
11.2
MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za
mishahara ya Serikali yaani TGS C Tsh: 201,870/= na kuendelea hadi Tsh:
250,930/= kwa mwezi.
11.3 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuingiza
kumbukumbu katika kompyuta
·
Kutoa
ushauri kwa wateja.
·
Kupokea,
kukagua na kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.
·
Kusaidia Maafisa Ardhi katika ukaguzi na
kuchukua kumbukumbu, picha taarifa, vipimo vya majumba na michoro.
·
Kujumuisha
na kuandaa taarifa za ukaguzi.
·
Kuandaa
rasimu za Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan)
·
Kuagiza
plani za Hati (Deed Plan)
12.0 DEREVA DARAJA LA II
(DRIVER II) – NAFASI 3
Nafasi
hizi ni kwa ajili yaMkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuendesha
magari ya abiria, magari madogo na malori
·
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika
hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari
ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
·
Kufanya
matengenezo madogo madogo katika gari,
·
Kutunza
na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
12.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato
cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha
magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti
cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).
12.3
MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGOS.A kwa mwezi.
13.0
AFISA UTALII DARAJA LA II – NAFASI 1
Nafasi
hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha.
13.1
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada
ya juu katika fani ya Utalii kutoka
katika
|
|
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
|
13.2
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
13.3
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye
vivutio vya utalii kwa kushirikiana na wadau wote.
·
Kutoa
Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii.
·
Kukusanya
na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii.
·
Kutafuta
na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi.
·
Kujibu
malalamiko kutoka kwa watalii.
·
Kutoa
ushauri wa kitaalam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii.
·
Kuandaa
kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii.
·
Kuchambua
miradi ya wakala wa utalii na hoteli.
·
Kukagua
hoteli, loji na migahawa.
·
Kujibu
na kufatilia malalamiko yanayoletwa na watalii.
·
Kutoa
ushauri wa kitaalam kwa wakala wa utalii.
·
Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye
vivutio vya utalii kwa kushirikiana na Washika dau wote.
·
Kukusanya takwimu za watalii kwenye
sehemu/vituo nchini vya kuingilia/kutoa wageni.
·
Kutunza
kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii.
·
Kutayarisha taarifa ya kila mwezi ya takwimu
za watalii waliongia nchini na mapato yaliyopatikana.
·
Kufanya tafiti ngo “Survey” kwenye Hifadhi za
Taifa na maeneo tengefu ili kupata idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa
huduma kwa watalii.
·
Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA
juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini.
·
Kuratibu
miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii.
·
Kutayarisha
ripoti za mwezi, robo mwaka, na za mwaka mzima.
·
Kufuatilia
kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya suervey.
·
Kuitisha
mikutano ya Tourism Facilitation Committee.
·
Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe
na kukufuatilia utekelezaji wa maazimio.
·
Kupitia
miongozo inayohusu “Tourism Facilitation Committee”.
·
Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii
na mienendo mipya ya kuendeleza utalii.
·
Kutayarisha
kuhakiki vivutio vya utalii nchini.
·
Kuitisha
mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii.
·
Kushiriki
katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii.
·
Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimali
za mazingira katika shughuli zihusuzo utalii na mazingira.
·
Kukusanya
rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.
14.0
AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE
OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi
hii ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
14.1
MAJUKUMU YA KAZI
12
·
Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi
vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )
·
Kuhamasisha
uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
·
Kukusanya
na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
·
Kutoa
ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
·
Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika
Shirikishi katika vyama vya ushirika vya Msingi.
14.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au
Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika (Cooperative
management and accounting) kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
14.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS D kwa mwezi.
15.0
AFISA SERIKALI ZA MITAA II (LOCAL
GOVERNMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala
Mkoa wa Shinyanga.
15.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa
ushauri katika utekelezaji wa Sheria za Serikali za Mitaa
·
Kutoa ushauri juu ya uanzishaji na uendeshaji
wa mamlaka mpya Serikali za Mitaa
·
Kutoa ushauri juu ya makadirio ya mapato ya
mapato na matumizi ya Seriakali za Mitaa
·
Kusimamia na kushauri juu ya matumizi bora ya
matumizi bora ya fedha Seriakali za Mitaa
·
Kutayarisha taarifa za robo mwaka na mwaka
zinazohusu mwenendo wa Serikali za Mitaa
·
Kufanya kazi nyingine zitakazoagiwa na
Watendaji, Wasimamizi wa masuala ya Serikali za Mitaa
15.2
SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya
kwanza ya Sanaa (/Management & Administration), Sheria (LLB) toka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali AU
13
·
Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu katika fani
ya Serikali za Mitaa au Utawala (Local Government Administration or Public
Administration) toka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
15.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya
Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
16.0
MHANDISI II UFUNDI (MECHANICAL ENGINEER)
– NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
16.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi
chini ya uangalizi
wa Mhandisi aliyesajiliwa
na bodi ya
usajili wa
Wahandisi kama Professional Engineer
ili kupata uzofu unaotakiwa.
·
Kufanya kazi kwa vitendo katika fani ya
Mekanika ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa
Wahandisi.
·
Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na
mitambo mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya
nchi.
·
Kupitia
mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya Ufundi .
16.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwawenye Shahada/Stashahada ya
juu ya Uhandisi
(Mechanical Engineering)
kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika na
Serikali.
16.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
17.0
MHANDISI II - HAIDROJIOLOJIA
(HYDROGEOLOGISTS) – NAFASI 4
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
17.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukusanya takwimu, kutafiti pamoja na
kutayarisha taarifa za
kihaidrojiolojia zenye
maelezo fasaha ya kitaalamu.
·
Kujenga (installation) na kukarabati vifaa
vya utafiti wa maji chini ya ardhi na kukarabati vituo vya kuratibu rasilimali
za maji chini ya ardhi.
·
Kusimamia uchumbaji wa visima vya maji na
kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji (pumping test)
·
Kukusanya
sampuli za maji na udongo kwa ajili kufanya uchunguzi wa kimaabara
·
Kutathimini (monitoring) rasilimali za maji
chini ya ardhi kwenye sehemu ya kidao cha maji (sub –catchment).
14
17.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye shahada ya Jiolojia au Jiofizikia na Haidrojiolojia kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.wawe na
ujuzi wa kutumia Kompyuta.
17.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
18.0 MHANDISI
DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE ENGINEER – NAFASI 50
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
18.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia
upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki
shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
·
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu
na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi,
uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na
usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
·
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi
na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
·
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa
miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
·
Kutayarisha
bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
·
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji
wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
·
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
18.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource
Engineering) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
18.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
19.0
MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER
RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
15
19.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia
upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki
shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
·
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu
na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi,
uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na
usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
·
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi
na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
·
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa
miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
·
Kutayarisha
bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
·
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji
wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
·
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
19.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with
GIS) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
19.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
20.0 MHANDISI DARAJA LA II (UMEME) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
20.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi
chini ya uangalizi
wa Mhandisi aliyesajiliwa
na bodi ya
Usajili wa
Wahandisi kama “Proffesional
Engineers” ili kupata uzoefu unaotakiwa.
·
Kufanya kazi za vitendo katika fani
zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi
ya Usajili wa Wahandisi.
·
Kukusanya taarifa za Magari na Mitambo
mbalimbali, kuhusu vifaa vya Umeme ndani na nje ya nchi.
·
Kupitia
mapendekezo ya miradi (Project proposals.) mbalimbali za Ufundi na Umeme.
20.2
SIFA ZA MWOMBAJI
16
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya
Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojwapo ya fani
ya Umeme (Electrical Engineering).
20.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
21.0
MHANDISI II MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL
ENGINEER II) – NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
21.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa
ushauri wa namna ya kulinda mazingira kutokana na shughuli za Binadamu
kama Kilimo,uvuvi,ufugaji nk
·
Kufanya Tathimini ya Mazingira (Environmental
Impact Assesment) kwa miradi inayoanzishwa hasa ya Umwagiliaji na Uwekezaji
katika Kilimo
·
Kutoa ushauri wa namna ya kupunguza uharibifu
wa Udongo utokanao na kemikali za madawa ya Kilimo, Pembejeo za Kilimo au
Kemikali zingine za Viwandani zihusianazo na kilimo.
·
Kubuni vifaa na mikakati ya kuhakikisha kuwa
maji taka na uchafu utokanao na kemikali zitokazo na Kilimo haziathiri
Mazingira.
·
Kubuni mikakati itakayohakikisha kuwa
Binadamu anaishi katika mazingira yenye Afya na Rafiki kimazingira.
21.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Stashahada ya juu au Shahada ya Uhandisi Mazingira kutoka Vyuo
Vikuu
au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia
compyuta.
21.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
22.0
FUNDI SANIFU DARAJA LA II – UFUNDI
(TECHNICIAN GRADE II MECHANICS) – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
22.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
·
Kufanya
upimaji wa Mitambo kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
·
Kufanya
kazi za kutengeneza mitambo na magari.
·
Kufanya
usanifu wa miradi midogo midogo ya ufundi.
17
·
Kusimamia
jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi.
22.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika
moja ya fani za ufundi.
Au
·
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya
ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali
katika mojawapo ya fani za ufundi,
Au
·
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya
I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
Au
·
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za
ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
22.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
23.0
FUNDI SANIFU DARAJA LA II - UMEME
(TECHNICIAN GRADE II ELECTRICAL) – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
23.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
ukaguzi wa ubora wa mitambo ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
·
Kufanya
upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
·
Kufanya
kazi za kutengeneza mitambo na vifaa vya
Umeme
·
Kufanya
usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme
·
Kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya
zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na Umeme.
23.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika
moja ya fani za ufundi umeme.
Au
·
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya
ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali
katika mojawapo ya fani za ufundi umeme,
Au
·
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya
I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
Au
·
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za
ufundi umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
18
23.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
24.0
FUNDI SANIFU – (WATER WORKS TECHNICIAN)
DARAJA II – NAFASI 124
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
24.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu Daraja I katika kazi ili kuapata uzoefu wa;
·
Kutafsiri ramani za ujenzi wa miundombinu ya
maji au ya ufungaji wa mitambo ya miradi ya maji
·
Kujenga miundombinu ya aina mbalimbali au
kufunga mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu wa miundo mbinu kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa
dharura;
·
Kusimamia ukusanyaji na utunzaji wa takwimu
za uendeshaji na matengenezo ya miundo mbinu au mitambo ya miradi ya maji;
·
Kuwaongoza
mafundi sanifu wasaidzi kutekeleza kazi zao
·
Kutoa
taarifa za utekelezaji wa miradi kwa Mhandisi
24.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Awe
na Cheti cha Stashahada ya Maji (Water Works Technician) toka Chuo cha Maji au
Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
24.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
25.0
FUNDI SANIFU MAABARA – (WATER LABORATORY
TECHNICIAN) DARAJA II – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
25.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu Daraja I katika kazi ili kuapata uzoefu wa;
·
Kutafsiri maelezo ya matumizi ya madawa
mbalimbali kwa kwa ajili ya kazi mbalimbali za maabara
·
Kusimamia
uchukuaji wa sampuli za maji na udongo kwa ajili ya upimaji
·
Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vya
maabara ya kawaida na ya dharura yanapohitajika;
·
Kufanya upimaji wa maji na udongo wa maeneo
ya miradi na kuandaa maelekezo ya matibabu yanayohitajika.
19
·
Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za hali ya
maji na udongo zinazohitajika kwenye maeneo ya miradi
·
Kuwaongoza
mafundi sanifu wasaidzi kutekeleza kazi zao
·
Kutoa
taarifa za hali ya maji na udongo wa maeneo ya miradi kwa Mhandisi.
25.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Awe
na Cheti cha Stashahada ya Maji (Water Laboratory) toka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
25.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
26.0
FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI -
(TECHNICIAN GRADE II - WATER) – NAFASI 1
Nafasi
hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
26.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Ukusanyaji
na ukaguaji wa takwimu za maji
·
Kutunza
takwimu za maji
·
Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H:
12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro
·
Kuchora
hydrograph za maji
·
Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za
winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k.
·
Kufanya
matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia
maji na hali ya hewa
·
Kuingiza
takwimu kwenye kompyuta
·
Kufundisha
wasoma vipimo
26.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na
Serikali ambao
|
|
wana
cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye
|
|
ujuzi wa kutumia kompyuta.
|
26.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
27.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI BOMBA) -
(ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN PLUMBING) – NAFASI 36
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
20
27.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga mitandao ya bomba za aina mbalimbali
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa mitandao ya bomba
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuwezesha uzalishaji na usambazaji wa maji na
utoaji wa majitaka kwa kupitia mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi nay
a kuzuia uharibifu wa mitandao ya bomba kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa
dharura.
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitandao ya bomba za
miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kumsaidia
Fundisanifu kazi za kiufundi.
27.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Plumbing).
27.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
28.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) -
(ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
28.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili
aweze;
·
Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na
kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za kupitisha bomba kwa ajili ya miradi
ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya
inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha
usanifu wa miundo mbinu miradi;
·
Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu
kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa
ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa
namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu wa miradi kufanya kazi
yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu wa
miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
21
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
28.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).
28.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
29.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI
(PAMPU) – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
29.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atafanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga
pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini
za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuhudumia
uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
·
Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi
ya maji;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
29.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).
29.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
30.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI
(UMEME) – NAFASI 25
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
30.1
MAJUKUMU YA KAZI
22
·
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya
uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
·
Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili
ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya
aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme,
mota na vifaa vingine umeme vya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili
ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
·
Kuendesha
mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa
kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
30.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
30.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
31.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN
WELDING) NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
31.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga
pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini
za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuhudumia
uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi
nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi
ya maji;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
23
31.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.
31.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
32.0 MHANDISI DARAJA LA II - UJENZI (ENGINEER
GRADE II – CIVIL) – NAFASI 125
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Katibu Mkuu Wizara ya
Maji.
32.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi
aliyesajiliwa (Professional engineer) na bodi ya usajili ya Wahandisi ili
kupata uzoefu unaotakiwa.
·
Kufanya
ukaguzi wa Barabara, Madaraja na Majengo mbalimbali
·
Kuchunguza
vyanzo vya ajali barabarani
·
Kufuatilia
utekezaji wa Sheria, Kanuni za ujenzi wa Barabara na Majengo
·
Kutayarisha bajeti ya mwaka ya Ujenzi na
matengenezo ya Barabara, Madaraja na Majengo
·
Kusimamia na kuratibu kazi za Barabara, Madaraja
na Majengo zinazotolewa na makandarasi
32.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya
Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi
Ujenzi.
32.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
33.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 36
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mkurugenzi
Mtendaji
Halmashauri
ya Wilaya ya Mkinga.
33.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
·
Kuchonga
vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
·
Kufanya kazi za upimaji ( Survey ) wa
barabara,majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa,
33.2
SIFA ZA MWOMBAJI
24
·
Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika
masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa
Ujenzi (Civil Technician ) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali,
Au
·
Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye
cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II (Civil Technician) kutoka chuo cha
ufundi katika mojawapo ya fani ya ufundi wa Ujenzi.
33.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
34.0
FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI
(TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING)
–
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
34.1
MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia
madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake
·
Kutunza kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake · Kuandaa nakala za
“cadastral site plans”
·
Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
34.2
SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye
cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)
34.3
MSHAHARA
·
.
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
35.0
MPIGA
CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) - NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza
‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha,
kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora.
·
Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au
majarida kwa kuyawekea gamba jipya, au kurudisha katika hali yake ya mwanzo
kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika.
25
·
Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika
makasha kwa vipimo vyake au katika seti.
·
Kuendesha mashine za kukata karatasi/kupiga
Chapa/Mashine za Composing, kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari
na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake.
·
Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya
kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.
35.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV
au VI katika masomo ya Sayansi, au Sanaa,
|
|
wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi
Daraja la I (Trade Test Grade I) katika
|
|
Lithography/Composing/Binding/Machine Minding,
au waliohitimu mafunzo
ya
|
|
miaka miwili ya Kupiga Chapa.
|
35.3
|
MSHAHARA
|
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi
wa Umma.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SERIKALINI MWISHO , 11 Julai, 2014
Reviewed by Unknown
on
11:29:00 AM
Rating: