Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 51 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
1.0 AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI 51
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.
• Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
• Kufanya ukaguzi wa viwanja.
• Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria.
• Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Usimamizi ardhi na
Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali
wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
v. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kupokea za maombi ni tarehe 05 Februari, 2015
xi. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au
Kiingereza na yatumwe kwenye mfumo wa elektroniki kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
xiii. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI
KWENYE SEHEMU YA ‘OTHER ATTACHEMENTS’
AJIRA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI - JAN 2015
Reviewed by Unknown
on
6:11:00 PM
Rating: