Kumb. Na
EA.7/96/01/H/34 23 Januari, 2015
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza
nafasi 121 za kazi kwa ajili ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa
serikali na Mamlaka za serikali za mitaa
1.0
AFISA MISITU DARAJA LA II (FOREST OFFICER GRADE II) –
NAFAS 5
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na
misitu.
·
Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa
isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
·
Kufanya
utafiti wa misitu.
·
Kutekeleza
Sera na Sheria za misitu.
·
Kuendesha
mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
·
Kukusanya
takwimu za misitu.
·
Kufanya
ukaguzi wa misitu.
·
Kupanga
na kupima madaraja ya mbao.
·
Kudhibiti
leseni na uvunaji wa miti.
·
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya
uendelezaji na matumizi endelevu
ya miti na kwa wananchi.
·
Kufanya
ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
·
Kupima
maeneo na kuchora ramani za misitu.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo
Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
1.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
2.0
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – NAFASI 7
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya
hifadhi
·
Kudhibiti
vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
·
Kusimamia
shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
·
Kulinda
binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
·
Kukusanya
na kulinda Nyara za Serikali
·
Kufanya
usafi na ulinzi wa kambi
·
Kusimamia
uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
·
Kukusanya
na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
·
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi
ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
·
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori
hai na nyara nje na ndani ya Nchi
·
Kudhibiti
wanyamapori waharibifu
·
Kudhibiti
moto kwenye hifadhi
·
Kufanya
kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
2.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato
cha VI wenye Astashahada au Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori
(Technician or Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo
cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
2.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS B1 kwa mwezi
3.1
AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE
OFFICER
GRADE III) – NAFASI 30
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha
Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
·
Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika
mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
·
Atakuwa
ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
·
Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli
za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.
·
Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa
sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia
shughuli za Uchaguzi katika Kata.
·
Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika
kusimamia maendeleo ya eneo lake.
·
Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na
watendaji wengine katika ngazi ya Kata.
·
Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na
kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
·
Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya
vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
·
Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote
zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
3.2
SIFA ZA MWOMBAJI.
·
Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita
na mwenye cheti cha Mafunzo ya Stashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu
ya Jamii (Sociology), Maendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango
kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au chuo chochote
kinachotambulika na Serikali.
3.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya
Mshahara TGS C kwa mwezi.
4.1
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 10
4.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kukusanya
takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
·
Kukusanya
takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
·
Kuendesha
mafunzo ya wataalam wa kilimo,
·
Kufanya
ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
·
Ufuatiliaji
wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
·
Kuendesha
mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
·
Kutoa
habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
·
Kuandaa/kuandika
taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
·
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji
mboga, matunda, maua na mazao mengine,
·
Kusimamia/kuendeleza
uzalishaji wa mbegu bora,
·
Kuandaa,
kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
·
Kufanya
majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
·
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa
kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,
·
Kuendesha
mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
·
Kuhamasisha
uzalishaji wa mazao ya bustani,
·
Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao
yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
·
Kufanya
utafiti wa udongo,
·
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya
wakulima/wamwagiliaji,
·
Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio
vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
4.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa
kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
4.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
5.1
AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD
OFFICERS)
–
NAFASI 12
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba
vya majaribio,
·
Kukusanya/kuhifadhi
takwimu za majaribio,
·
Kuwafundisha
wakulima mbinu za kilimo bora,
·
Kuwafikishia
wakulima matokeo ya utafiti,
·
Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo,
matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei
kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri,
·
Kukusanya
takwimu za mvua,
·
Kushiriki
katika savei za kilimo,
·
Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu
matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,
·
Kupanga
mipango ya uzalishaji,
·
Kupima
uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
·
Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya
maji kwa ajili ya kuhifadhi,
·
Kutunza
miti mizazi,
·
Kuwatambua
wasambazaji wa pembejeo,
·
Kutoa
mafunzo ya lishe kwa wakulima,
·
Kufanya
vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
·
Kusimamia
taratibu za ukaguzi,
·
Kudhibiti
visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kusimamia
shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
·
Kuwaelimisha
wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
·
Kutoa
ushauri wa kilimo mseto,
·
Kuandaa
sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
·
Kutoa
taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne au Sita
(VI) wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.
5.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
6.1
MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) – NAFASI 5
6.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa
kukusanya na kuratibu takwimu
·
Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu
pamoja na ule wa kuchukua takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)
·
Kukusanya,
Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani
ya Takwimu au Hisabati au sifa zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia Kompyuta.
6.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS D kwa mwe
7.1
AFISA UGAVI MKUU DARAJA LA I - NAFASI 1(INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa
Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)
7.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushauri juu ya Sera ya Ununuzi na Ugavi
katika Wakala;
·
Kushauri juu ya Mfumo wa Mtandao wa Ununuzi
na Ugavi kwa kutumia kompyuta,
“e-procurement”;
·
Kutathmini taarifa ya vifaa vinavyotumika na
Wakala ili kujua aina ya kasi ya vifaa husika kwa hatua zaidi;
·
Kusimamia utayarishaji wa Mpango wa manunuzi
wa Wakala;
·
Kusimamia
utayarishaji wa makisio ya vifaa vinavyohitajika katika Wakala;
·
Kusimamia
upimaji wa utendaji wa Maafisa Ugavi walio chini yake;
·
Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora
kutekeleza majukumu yanayohusu ununuzi, utunzaji na ugavi katika Wakala;
7.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Ugavi na
Shahada/Stashahada ya Uzamili katika fani za Biashara au Ugavi kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa, na uzoefu wa kazi
usiopungua miaka kumi na mbili (12).
7.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali
yaani WMAS 7 kwa mwezi
8.0
AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 1 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa
Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)
1.1.2
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kukagua,
kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
·
Kutunza
na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
·
Kutoa
ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
·
Kufanya
upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo;
·
Kupokea
na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;
1.1.3
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika
fani ya Legal Metrology au Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali. Au
·
Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya
Uhandisi / Sanyansi ambao wamepata crash programme in Legal and Industrial
Metrology isiyopungua miezi mine (4) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Au
·
Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya
Uhandisi / Sayansi ambao wamehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate
Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
·
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu katika
fani ya Legal Metrology / Legal and Industrial Metrology kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.4
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS3 kwa mwezi.
9.1
MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER
RESOURCE ENGINEER – NAFASI 6 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maji na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
9.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa
ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji
maji na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na
matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu
na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi,
uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na
usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
·
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi
na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
·
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa
miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
·
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji
wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
·
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
9.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya
uhandisi wa Maji (Water Resource Engineering) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
9.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS E kwa mwezi.
10.1
FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI
(UMEME) – NAFASI 15 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
10.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya
uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
·
Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili
ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina
mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme,
mota na vifaa vingine umeme vya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili
ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
·
Kuendesha
mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa
kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
10.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III
(Plants Technician Electrical).
10.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
11.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT
TECHNICIAN - WATER) NAFASI 24 (INARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
11.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kupima uwingi wa maji mtoni
·
Kusoma
kituo cha hali ya hewa
·
Kazi
nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
11.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka kutoka Chuo cha Maji au
Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja
la III katika fani ya maji.
11.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
12.1
MHANDISI KILIMO II (IRRIGATION) - 1
12.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima
kutumia zana za kilimo.
·
Kushiriki
katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
·
Kushiri
katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji.
·
Kukusanya
takwimu za miradi ya umwagiliaji.
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji.
·
Kuandaa
mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.
·
Kuwafundisha
wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.
·
Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
12.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu
kinachotambuliwa na serikali.
12.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS E kwa mwezi
13.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima
kutumia zana za kilimo.
·
Kushiriki
katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
·
Kushiri
katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji.
·
Kukusanya
takwimu za miradi ya umwagiliaji.
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji.
·
Kuandaa
mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.
·
Kuwafundisha
wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.
·
Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
13.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya zana za kilimo kutoka chuo kikuu
kinachotambuliwa na serikali.
13.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS E kwa mwezi
14.0
MHANDISI KILIMO II (LAND USE PLANNING) – 1
14.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa
programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.
·
Kushiriki
katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.
·
Kushiri
katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji.
·
Kukusanya
takwimu za miradi ya umwagiliaji.
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji.
·
Kuandaa
mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.
·
Kuwafundisha
wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.
·
Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
14.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya matumizi bora ya ardhi (land use planning)
kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali.
14.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E wa mwezi
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe
maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani
na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND
FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA).
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 Febuari,
2015
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
TANGAZO LA KAZI UTUMISHI - KISWAHILI - 23 Januari, 2015
Reviewed by Unknown
on
8:32:00 AM
Rating: