Kumb. Na EA.7/96/01/E/26 27
Novemba, 2013
TANGAZO LA NAFASI ZA
KAZI
Sekretariati
ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa
Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria
Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 2748 za kazi kwa ajili
ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo,Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya
Kinondoni.
Nafasi
nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Bukoba,
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji
Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Muheza.
Nafasi
hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.
Waajiri
wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya
Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.
Nafasi
hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya
Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi
Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Hai.
Katika
nafasi hizo waajiri weengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Bahi,
Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi
Halmashauri Manispaa ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala
Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu
Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa Ruvuma,
Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es
salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa
Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Simiyu na Katibu Tawala
Mkoa Geita.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii.
Waombaji
wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika
kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha
maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatanishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato
cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional
certificates from respective boards)
vii.
“Transcripts”, “Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji
wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES
SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO
MENGINE.
xiii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Desemba,
2013
xiv.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi.
Kila mwombaji kazi atapangwa katika
kituo chochote cha kazi bila kujali eneo/mahali alipoomba kutokana na mahitaji
ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo husika.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
1.0
AFISA UVUVI DARAJA LA II (FISHERIES OFFICER GRADE II) –
NAFASI 39
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutekeleza Sera ya Uvuvi.
·
Uhifadhi
wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao.
·
Kuratibu
na kusimamia uhifadhi wa mazingira.
·
Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na
viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito, mabwawa na malambo.
·
Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu Uvuvi bora,
utengenezaji na udhifadhi bora wa Samaki na mazao ya uvuvi, Biashara na Masoko
ya Samaki pamoja na Ufugaji wa Samaki na viumbe wengine wa majini.
·
Kutoa
leseni za uvuvi.
·
Kuendesha
mafunzo ya taaluma ya uvuvi.
·
Kusimamia
na kutekeleza Sheria za Uvuvi (k.m. kuzuia uvuvi haramu).
·
Kusimamia
ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli.
·
Kuratibu
shughuli za utafiti wa uvuvi.
·
Kutoa ushauri na Mafunzo kwa wananchi juu ya
uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya uvuvi.
·
Kukagua
ubora wa Samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya Kitaifa.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (Bachelor
Degree) katika fani za Sayansi ya Uvuvi (Fisheries Science/Management, Zoology,
Microbiology, Marine Biology, Food Science and Aquaculture).
1.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 MVUVI MSAIDIZI DARAJA
LA II (FISHERIES ASSISTANT II) – NAFASI 18
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati
zana za uvuvi.
·
Kutunza
na kuangalia mabwawa ya samaki.
·
Kutega
mitego Ziwani au Baharini.
·
Kutengeneza
nyavu ndogo ndogo.
·
Kuwapa
chakula samaki katika mabwawa.
·
Kuvua
samaki katika mabwawa.
·
Kutoa
ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi.
·
Kukusanya
takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki.
·
Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na
mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na samaki.
·
Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa
samaki na mambo muhimu ya kuzingatia.
2.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha
sita wenye stashahada (Diploma) ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish
Processing & Marketing) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo
vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS C kwa mwezi
3.0 AFISA
MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II) – NAFASI 473
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa
wafugaji wa eneo lake.
·
Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya,
atakagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara.
·
Atakusanya takwimu za nyama na mazao
yatokanayo na mifugo k.m ngozi na kuandika ripoti.
·
Atatibui magonjwa ya mifigo chini ya
usimamizi wa Daktari wa mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo
dhidi ya magonjwa.
·
Atatembelea wafugaji mara Kwa mara na kuwapa
ushauri fasaha wa kitaalam katika eneo Lake Kazi.
·
Atakusanya
takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake .
·
Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho,
machinjio, vibanio na miundo mbinu inayohusiana na ufugaji bora.
·
Atahusika na uhamilishaji (Artificail
Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa ujumla.
·
Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha
maziwa na utunzaji wa ndama.
·
Atafanya kazi nyingine za fani yake kama
atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
3.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu
mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo
(MATI au LITI) au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
3.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS C kwa mwezi
4.0 AFISA MIFUGO DARAJA
LA II (LIVESTOCK OFFICER II) – NAFASI 107
4.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo
wilayani.
· Ataratibu uzalishaji
wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
·
Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji
bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
·
Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya
masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
·
Atabuni,
kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
·
Atafanya soroveya ya rasilimali (resource
survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la
kazi.
·
Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na
wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
·
Atatafiti
maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
·
Atafanya
utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
·
Atashiriki katika shughuli za kudhibiti
milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
·
Ataandaa
taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
·
Atafuatilia,
kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
·
Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani
yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
4.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya sayansi ya Mifugo
(Animal
Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana
nayo.
4.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi
5.0 MTEKNOLIJIA
WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGISTS II) – NAFASI 4
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa ushauri juu ya utayarishaji,
utengenezaji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki na mazao yatokanayo na uvuvi.
·
Kusimamia
kushauri juu ya kanuni za uthibiti ubora wa Samaki na mazao yake
·
Kutoa ushauri juu ya matumizi mbalimbali ya
samaki kama chakula bora katika Viwanda na maeneo mengine.
·
Kudhibiti
ubora wa samaki katika mialo.
·
Kudhibiti
usafi katika maeneo ya kupokelea samaki.
·
Kukagua
nyaraka mbalimbali zinazotakiwa kutunzwa melini na viwandani.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya Sayansi ya Chakula (Food Science and Nutrition, Food Technology,
Microbiology) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi
6.0 DAKTARI WA MIFUGO DARAJA
LA II (VETERINARY OFFICERS) – NAFASI 19
6.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa huduma za afya ya mifugo
·
Kufanya
uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo au sehemu alipo.
·
Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia,
kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
·
Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya
wanyama pori katika eneo lake.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya Tiba ya Mifugo
kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
6.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS E kwa mwezi
7.0 AFISA
UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 9
7.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kujifunza kumudu mbinu na taratibu za utafiti
wa mifugo/ndorobo
·
Kufanya
utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
·
Kuandika
na Kuweka kumbukumbu za utafiti.
·
Kusaidia
kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
·
Kuandaa mapendekezo ya utafiti (Research
Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayesimamia.
·
Kufanya
kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
7.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
7.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS D kwa mwezi
8.0 DAKTARI
UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 5
8.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kujifunza na kumudu mbinu na taratibu za
utafiti wa afya na maradhi ya mifugo
·
Kuweka
kumbukumbu za utafiti
·
Kusaidia
kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
·
Kuandaa mapendekezo
ya utafiti (“research
proposal”) kwa kushirikiana
na
Daktari
Utafiti Mifugo anayemsimamia.
·
Kufanya
utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
·
Kukusanya
na kuchambua takwimu za utafiti unaoendelea.
·
Kuchapisha
taarifa na makala za utafiti
·
Kuendesha
semina na maonyesho ya ufugaji bora.
8.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor
degree) katika fani ya Sayansi
ya Tiba ya Mifugo (“Veterinary
Science) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo
au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya
Madaktari wa Mifugo nchini.
8.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS E kwa mwezi
9.0
FUNDI SANIFU MAABARA MIFUGO DARAJA LA II
(VETERINARY LABORATORY TECHNICIAN II) – NAFASI 6
9.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kwa kushirikiana na Afisa Mifugo Msaidizi,
atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
·
Atakusanya
sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara.
·
Kuwasaidia
wataalam kuanda vifaa vya uchunguzi
·
Kutunza
Usafi wa Maabara na vyombo vilivyomo.
·
Kutunza
takwimu za uchunguzi
·
Atafanya
kazi zingine zozote kama atavyopangiwa na mkubwa wake wa kazi
9.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita (VI)
waliofuzu mafunzo ya miaka miwili (2)
ya
Stashahada katika fani ya Fundi Sanifu Maabara (Mifugo) kutoka Chuo cha Mifugo
(LITI), au chuo kingine kinachotambiliwa na serikali.
9.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
TGS C kwa mwezi
10.0
MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (LIVESTOCK TUTOR II) – NAFASI 5
10.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye
masomo.
·
Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson Plan)
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kufundisha kozi za stashahada na astashahada
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendelo ya wanachuo kwa kushirikiana
na maofisa mifugo wa wilaya, viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo.
·
Kufanya kazinyingine zozote za fani yake
atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
10.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
10.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
11.0 MKUFUNZI
WA MIFUGO MSAIDIZI (ASSISTANT LIVESTOCK TUTOR) – NAFASI 3
11.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa mtiririko (Lesson Plan) wa masomo
·
Kufundisha
kozi ya astashahada ya mifugo na wafugaji.
·
Kusimamia
masomo ya vitendo chini ya usimamizi wa Mkufunzi Mkuu wa somo
·
Kuandaa
na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo
·
Kuwapima
wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo
·
Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo
(dairy, poultry, maabara, museum, nk).
·
Kufanya
kazi nyingine kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
11.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (VI)
waliofuzu mafunzo ya Stashahada ya mifugo kutoka MATI/LITI au chuo kingine
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
11.3
MSHAHARA
12.1 DAKTARU
MIFUGO MKUFUNZI DARAJA LA II (VETERINARY TUTOR II) – NAFASI 1
12.2
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
·
Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan)
kwa upande wa nadharia na vitendo
·
Kufundisha kozi za stashahada na astashahada
kwa upande wa nadharia na vitendo.
·
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na
kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani
kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
·
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana
na madaktari /maofisa mifugo wa wilaya, wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field
Practicals).
·
Kufanya
kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
12.3
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi
ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari Tanzania.
12.4
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
13.0 MTEKINOLOJIA
WA SAMAKI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT FISH TECHNOLOGIST II) – NAFASI 6
13.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutengeneza
na kuhifadhi samaki
13.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita
waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya uhifadhi na biashara ya samaki (Fish
Processing and Marketing) kutoka chuo cha maendeleo ya uvuvi Mbegani au chuo
chochote kinachotambuliwa na serikali.
13.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi
14.0
MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2
14.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusaidia kuunda boti za uvuvi
·
Kuwashauri
wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
·
Kusaidia
kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
·
Kuandaa
vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
14.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye stashahada ya Uundaji boti
kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
14.3
MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
15.0
DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY /
BOAT OPERATOR) – NAFASI 1
15.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
·
Kuchunga
usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
·
Kupanga
abiria au magari kwenye kivuko.
·
Kuendesha
na kuongoza kivuko.
·
Kutunza
daftari za safari ya kivuko.
·
Kuhakikisha
kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
·
Kuangalia
mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
15.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha
IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo
cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na
Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita
ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye
mashua/vivuko.
15.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
16.0
MSAIDIZI MIFUGO (LIVESTOCK FIELD ASSISTANTS) – NAFASI 209
16.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji
mifugo na mazao yake,
·
Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa,
tiba na chakula,
·
Kusimamia utendaji kazi wa wahudumu mifugo,
·
Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za
mifugo,
·
Kusimamia ustawi wa wanyama,
·
Kufanya kaza nyingine atakazo pangiwa na
msimamizi wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.
16.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV ambao
wamepata mafunzo ya mifugo ya muda wa miaka miwili na kutunukiwa Astashahada
(certificate) ya uzalishaji na afya ya mifugo kutoka vyuo vya mafunzo ya
mifugo. (Livestock Training Institute
–
LITI) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
16.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.
17.0
AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 200
17.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki
na kila mwezi,
·
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao
katika masoko kila wiki/kila mwezi,
·
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
·
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya
pembejeo na zana,
·
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya
biashara,
·
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya
udongo na maji,
·
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa
wadau,
·
Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta
ndogo ya mazao,
·
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji
mboga, matunda, maua na mazao mengine,
·
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu
bora,
·
Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza
mbegu bora,
·
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
·
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa
kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,
·
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga,
matunda, maua na viungo,
·
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
·
Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao
yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
·
Kufanya utafiti wa udongo,
·
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya
wakulima/wamwagiliaji,
·
Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa
na watafiti,
·
Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio
vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
17.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa
kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
17.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
18.0
AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD
OFFICERS)
–
NAFASI (1098)
18.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba
vya majaribio,
·
Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,
·
Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,
·
Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,
·
Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo,
matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei
kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri,
·
Kukusanya takwimu za mvua,
·
Kushiriki katika savei za kilimo,
·
Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu
matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,
·
Kupanga mipango ya uzalishaji,
·
Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu
za ukaguzi,
·
Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya
maji kwa ajili ya kuhifadhi,
·
Kutunza miti mizazi,
·
Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,
·
Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,
·
Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na
uotaji wa mbegu,
·
Kusimamia taratibu za ukaguzi,
·
Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,
·
Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio
ya kilimo,
·
Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya
udongo na maji,
·
Kutoa ushauri wa kilimo mseto,
·
Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira
na
·
Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga,
matunda, maua na viungo.
18.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI)
wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.
19.0
MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI
82
19.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima
kutumia zana za kilimo,
·
Kushiriki katika kufundisha wakulima na
matumizi bora ya zana,
·
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za
umwagiliaji,
·
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya
umwagiliaji,
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
·
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
·
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za
za kilimo,
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
·
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora
na
·
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
19.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor
Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji
na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
19.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
20.0
FUNDI SANIFU DARAJA LA II – NAFASI 74
20.1
MAJUKUMU YA KAZI
Fani ya Kilimo
·
Kutoa ushauri kwa wakulima kuhusu matumizi
bora ya zana za kilimo kwa vitendo,
·
Kuwafundisha wakulima kutengeneza na kufanya
matengenezo ya zana za kilimo,
·
Kuendeleza kilimo cha zana,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za zana za
kilimo,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za kilimo cha
umwagiliaji,
·
Kusaidia katika ujenzi wa mifereji ya
umwagiliaji,
·
Kushiriki katika savei kwa ajili ya kilimo
cha umwagiliaji,
·
Kushiriki katika ujenzi wa malambo madogo.
Fani ya Maabara
·
Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili
kuthibitisha/kutathmini udongo, mimea na mbolea na vielelezo (samples)
vinavyohusika kwenye maabara.
·
Kutunza vyombo vya maabara,
·
Kutunza kumbukumbu za maabara,
·
Kutambua, kuthibitisha na kuweka kumbukumbu
za takwimu za vidudu mbalimbali vinavyosababisha magonjwa ya mimea,
·
Kusaidia kaza za watafiti,
·
Kwenda mashambani kuchukua sampuli
zinazohitajika kwa uchunguzi katika maabara.
20.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato
cha Sita (VI) waliofuzu mojawapo ya mafunzo yafuatayo:
·
Mafunzo ya miaka miwili (2) ya stashahada
(Diploma) ya ufundi sanifu wa vyombo vya kilimo (agro-mechanics), au ufundi
sanifu Umwagiliaji maji, na `Agricultural land use technician`
·
Mafunzo ya miaka miwili (2) ya stashahada
(Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara,
·
Mafunzo ya Taasisi za ufundi (VETA)
·
Au sifa zinazolingana na hizo kutoka kaitka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
20.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
21.0 AFISA
UTAFITI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURAL RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 24
21.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za
utafiti wa kilimo/uchumi kilimo chini ya maelekezo ya afisa utafiti mwandamizi,
·
Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za
kazi za utafiti zinazoendelea,
·
Kuhudhuria mikutano ya Kanda ya kuhuisha
programu za utafiti,
·
Kusaidia katika kuendesha semina na
kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia teknolojia mpya kwa kuzingatia hali ya
uchumi na mazingira yao,
·
Kutoa ripoti ya maendeleo ya utafiti na
mapendekezo ya utafiti katika mikutano ya kanda ya kuhuisha program za utafiti,
·
Kufanya shughuli za utafiti chini ya
maelekezo na uangalizi wa afisa utafiti mwandamizi,
·
Kuandika mapendekezo ya utafiti chini ya
uongozi wa afisa utafiti mwandamizi,
·
Kuandika ripoti za miradi ya utafiti kwa
ajili ya kupitishwa na afisa utafiti mwandamizi,
·
Kufanya majaribio ya husishi ya kilimo ma
mifugo katika mashamba ya wakulima kwa kushirikiana na Maafisa Ugani na
wakulima wenyewe na
·
Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor
degree) ya Kilimo/Uchumi Kilimo/Uhandisi Kilimo, au sifa inayolingana na hizo
kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
21.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
22.0
MKUFUNZI WA KILIMO MSAIDIZI (AGRICULTURAL TUTOR) – NAFASI
22
22.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa mtiririko wa mpangilio wa masomo
(lesson sequences and plans),
·
Kuandaa na kufundisha masomo ya kozi za
astashahada,
·
Kusimamia masomo ya vitendo vya kozi za
stashahada chini ya usimamizi wa mkufunzi mkuu wa somo,
·
Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la
vitendo kwa kozi stashahada,
·
Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo
la vitendo kwa kozi za astashahada,
·
Kupima maendeleo ya wanachuo wa astashahada
kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao na
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
22.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita
waliofuzu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya Kilimo kutoka MATI au chuo kingine
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
22.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
23.0
AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III (AGRICULTURAL FIELD
OFFICERS)
–
NAFASI 362
23.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba
ya majaribio na mashamba darasa,
·
Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima
katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za
kisasa za kilimo cha kibiashara,
·
Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya
matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo,
·
Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya
kilimo katika kijiji,
·
Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya
hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao,
·
Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo
visumbufu vya mimea na mazao,
·
Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika
kutekeleza majukumu yake ya kila siku,
·
Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na
vikwazo vya maendeleo (Opportunities and Obstacles for Development (O & OD)
na kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural
Development Plan (VADP), na
·
Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi
kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji
wa Kijiji.
23.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye
stashahada (Diploma) ya Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
23.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.
24.0
DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 100
24.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na
malori
·
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika
hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari
ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
·
Kufanya
matengenezo madogo madogo katika gari,
·
Kutunza
na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
24.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato
cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha
magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti
cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).
24.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya
Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
25.0
MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 2.
25.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi
inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
·
Kuhahikisha
kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
·
Kulinda
usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
·
Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote
yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
·
Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia
katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
·
Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea
katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika.
·
Kutoa
ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
25.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne
waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali.
25.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
2.0 BARAZA LA KISWAHILI
LA TAIFA (BAKITA)
Baraza
la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria
ya Bunge Na 27 ya mwaka 1967.
2.1
MHASIBU MKUU DARAJA II - NAFASI 1
2.1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuratibu kazi ya kujibu hoja za ukaguzi.
·
Kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.
·
Kuandaa na kuoanisha taarifa za mwezi za
Benki.
·
Kuandaa taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka.
·
Kusimamia, kuthibitisha na kuidhinisha
malipo.
·
Kufanya kazi zingine kama atakavyoagizwa na
msimamizi wake wa kazi.
2.1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili ya
Uhasibu/ Biashara yenye mwelekeo wa Uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyote
inayotambuliwa na Serikali.
·
Awe na CPA (T).
·
Mwenye uwezo wa kutumia mifumo ya kompyuta ya
kiuhasibu.
·
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane
(8) mfululizo katika fani ya uhasibu.
2.1.3
MSHAHARA: PGSS 17
2.2
MSANIFU LUGHA MKUU III - NAFASI 1 2.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya utafiti kuhusu istilahi za masomo na
kukusanya mapendekezo ya istilahi za Nyanja nyinginezo.
·
Kusimamia mawasiliano baina ya Taasisi na
wadau wanaohitaji huduma za kusanifu Istilahi au msamiati.
·
Kusimamia kazi za utayarishaji wa tafsiri sanifu.
·
Kuratibu Warsha, Semina na Mikutano ya Kamati
ya Usanifishaji.
20
·
Kusimamia kazi ya kukusanya na kuchambua
istihali mbalimbali kwa ajili ya usanifishaji.
·
Kuratibu shughuli za Usanifishaji Lugha.
·
Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Idara.
·
Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na mkuu
wake wa kazi.
2.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa mwenye Shahada ya
Uzamili/Uzamivu katika masomo ya Fasihi, Lugha au Isimu ya Kiswahili
·
Awe na uzoefu wa kazi katika fani hiyo usiopungua miaka minane (8). ·
Awe na uwezo wa kutumia kompyuta
· Awe ameandika makala au
kitabu kinachohusu fasihi au isimu ya lugha ya Kiswahili.
2.2.3 MSHAHARA: PTSS 17
3 .0 WAKALA WA VIPIMO
Wakala
wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na
Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria za Serikali Sura Na. 245,
mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002
kwa amri ya Seriakali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe
17 Mei, 2002. Chini ya sheria hiyo, Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda
malaji Kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya,
Usalama na Mazingira
3.1 AFISA VIPIMO II – NAFASI 2 3.1.1 MAJUKUMU
YA KAZI
·
Kukagua,
kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
·
Kutunza,
kuhifadhi vifaa vya kitaalam vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
·
Kutoa
ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
·
Kufanya
upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Vipimo
·
Kupokea
na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na waateja;
·
Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na
kiongozi wake zinazohusiana na elimu na ujuzi wa kazi
3.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani
ya “Legal Metrology” au “Legal and Industrial Metrology” toka katika Chuo
kinachotambuliwa na Serikali. Au
·
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza ya Uhandisi/Sayansi ambao wamepata
“Crash
programme” ya “Legal and Industrial Metrology” isiyopungua miezi minne
(4)
toka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya
Uhandisi/Sayansi ambao wamehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma)
katika fani ya vipimo katika Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
·
Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu katika fani
ya “Legal Metrology” /Legal and “Industrial Metrology” toka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
3.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali ngazi ya mshahara (WMAS 3) kwa mwezi.
X. M. DAUDI
KATIBU- SEKRETARIETI YA AJIRA
NAFASI ZA KAZI UTUMISHI NOV 2013
Reviewed by Unknown
on
6:51:00 AM
Rating: