Loading...

NAFASI ZA KAZI Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imeanzishwa chini ya Sheria Namba 7 ya mwaka 1996 ikiwa ni Taasisi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na vianzio vya ndani.
Katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali, ZRB imekusudia kujaza nafasi mbalimbali zikiwemo:

Software Developer / Engineer
(4 Post Unguja and 1Post Pemba)
AFISA HABARI NA MAHUSIANO DARAJA LA II NAFASI MBILI (2) KWA AFISI YA ZRB UNGUJA
AFISA RASILIMALI WATU DARAJA LA II NAFASI (2) KWA OFISI YA ZRB UNGUJA.
MHUDUMU WA SIMU DARAJA LA III NAFASI MOJA (1) KWA OFISI YA ZRB UNGUJA
Afisa Mhasibu Daraja La Ii Nafasi Tatu (3) Kwa Ofisi Ya Zrb Unguja
 AFISA UNUNUZI NA UGAVI DARAJA LA II NAFASI MBILI (2) KWA OFISI YA ZRB UNGUJA
AFISA MAPATO DARAJA LA II NAFASI KUMI NA NNE (14)
Nafasi kumi (10) kwa Afisi ya ZRB Unguja na nafasi nne (4) kwa Afisi ya ZRB Pemba.

SIFA ZA MUOMBAJI
• Awe Mzanzibari
• Awe na elimu na Shahada ya kwanza au Diploma ya juu katika fani ya Kodi, Uhasibu,Uchumi na Biashara. kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na uwezo wa kutumia Computer
• Mwenye uelewa mzuri wa “Accounting packages” mbalimbali kama vile MYOB, PASTEL, QUIKBOOK n.k. atapewa kipaumbele.
• .Awe na umri usiozidi miaka 35.
• Awe mbunifu na awe na uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa
KAZI ZAKE
a. Kupokea ritani za walipakodi, pamoja na kuweka kumbukumbu zinahusika na kufanya uhakiki wa nyaraka hizo na kuzihifadhi.
b. Kukagua kumbukumbu na taarifa za mlipakodi ili kuhakikisha kodi sahihi inalipwa kwa mujibu wa sheria.
c. Kufanya uhakiki wa madai ya kodi (claims).
d. Kuainisha na kutathmini maeneo hatarishi ya upotevu wa mapato na kupendekeza hatua za kuchukuliwa
e. Kutoa mapendekezo ya kufanywa ukaguzi na upelelezi kwa mlipakodi.
f. Kusimamia na kufuatilia nafuu maalum ya Kodi.
g. Kutoa mapendekezo juu ya usimamizi bora kwa walipakodi kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
h. Kazi yoyote atakayepangiwa na Mkuu wake wa kazi.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua ya maombi iambatanishwe na maelezo binafsi (CV) inayoonesha wadhamini wawili na namba zao za simu, namba ya simu ya muombaji,kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari, Vyeti vya kumalizia Masomo,cheti cha kuzaliwa na picha mbili.(2) za passport size zilizopigwa karibuni.
Maombi yote yawasilishwe makamo makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar kwa kutumia anuwani iliyopo hapa chini si zaidi tarehe 22/4/2016.

KAMISHNA,
BODI YA MAPATO ZANZIBAR
P.O.BOX 2072, MAZIZINI
ZANZIBAR.

Newer Posts Older Posts
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

LIKE US ON FACEBOOK

© Copyright KaziBongo | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top