Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu
waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe
12/05/2015 hadi tarehe 29/05/2015 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo
vya kazi umekamilika.
Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana
katika Tangazo hili. Katika orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi
ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali
ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda
ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa
na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne
na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za posta.
Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa
mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
KUITWA KAZINI JUNE 2015 (Placements)
KUITWA KAZINI JUNE 2015 (Placements)
KUITWA KAZINI JUNE 2015 (Placements)
Reviewed by Unknown
on
2:04:00 AM
Rating: