VOLUNTEERING TRAINING OPPORTUNITIES " NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI "
RafikiElimu Foundation kupitia mradi wake EUV Project " Elimu Ya Ujasiriamali Vijijini " inatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu wa ujasiriamali kwa watanzania wenye sifa zifuatazo :
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Umri miaka kumi na nane hadi thelathini na tano.
2. Elimu kuanzia kidato cha nne , sita na kuendelea.
3. Awe raia wa Tanzania
4. Awe tayari kufanya kazi kama mwalimu wa ujasiriamali vijijini katika wilaya yoyote ya Tanzania bara atakayo pangiwa na asasi.
Mafunzo Yatakayo Tolewa
Kwa watakao pata nafasi ya kushiriki katika mafunzo haya wata jifunza mambo yafuatayo:
i. Utengenezaji wa sabuni.
ii. Utengenezaji wa mishumaa.
iii. Utengenezaji wa chaki.
iv. Utengenezaji wa viatu vya ngozi.
v. Usindikaji wa vyakula na matunda.
vi. Uongozi wa biashara
Muda Wa Mafunzo:
Mafunzo haya yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia tarehe 01 Septemba 2012 hadi tarehe 31 Septemba 2012.
ADA YA MAFUNZO : Ada ya mafunzo ni shilingi Elfu Ishirini na Tano Tu ( Tshs 25,000/=)
MALIPO YA ADA YA MAFUNZO : Malipo ya ada ya mafunzo yafanyike kupitia
Account Number : 0152395997900 , CRDB BANK
Account Name : RafikiElimu Foundation
DHUMUNI LA MAFUNZO :
Dhumuni la mafunzo ni kuwajengea washiriki uwezo wa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo wadogo waliopo maeneo ya vijijini.
MUDA WA MAFUNZO
Mafunzo yataanza rasmi tarehe 3 Septemba 2012 , na yatafanyika katika miji ya
Dar Es salaam, Arusha , Mwanza, Mbeya, Dodoma, Moshi na Tanga.
Mafunzo yatakuwa ni kwa nadharia na vitendo
WALENGWA WA MAFUNZO :
Walengwa wa mafunzo ni vijana walio hitimu kidato cha nne, cha sita na kuendelea ambao wanapenda kufanya kazi kama volunteers katika mradi wa Elimu Ya Ujasiriamali Vijijini na ambao wapo tayari kutumia muda wao kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo wadho waliopo maeneo ya vijini nchini Tanzania.
BAADA YA MAFUNZO
Baada ya mafunzo, vijana watakao pata nafasi ya kushiriki katika mafunzo haya na kufuzu vizuri watapewa nafasi ya kufanya kazi na asasi kama wawezeshaji ama walimu wa mafunzo ya ujasiriamali katika maeneo ya vijijini ambako muhusika atapangiwa na asasi.
KUHUSU MRADI
Mradi wa Elimu Ya Ujasiriamali Vijijini ni mradi unao ratibiwa na kusimamiwa na asasi ya RafikiElimu Foundation kwa msaada wa mashirika mbalimbali. Dhumuni la mradi ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wajasriamali wadogo wadogo wapatao 5000 waliopo katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania kwa kuwatumia vijana wa kitanzania waliopata mafunzo ya kuwawezesha kufanya kazi kama walimu wa ujasiriamali.
MAOMBI : Tuma barua yako ya maombi , ambatanisha na C.V yako, nakala ya cheti chako cha kuzaliwa ama/ nakala ya kadi ya mpiga kura, pamoja na nakala ya risiti ya malipo ya ada ya mafunzo kwenda kwa
Meneja Mradi,
Elimu Ya Ujasiriamali Vijijini
c/o RafikiElimu Foundation,
S.L.P 35967,
Dar Es salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Agosti 2012. .
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu : 0714728415 au 076397654
Application Instructions:
.
kwa maelezo zaidi tembelea : www.rafikielimu.blogspot.com
Start Date: Sep 03, 2012
No comments: