Loading...

NAFASI ZA KAZI Lodhia Steel Industries Limited

Lodhia Steel Industries Limited
NAFASI ZA KAZI
NAFASI ZA KAZI ZINAPATIKANA KATIKA KIWANDA CHAO CHA KUTENGENEZA NELI (TUBEMILL PLANT) KILICHOPO KISEMVULE, WILAYA YA MKURANGA
Tanakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watu waliohitimu na wenye ujuzi na uzoefu katika nafasi zifuatazo:
Wasimamizi (nafasi tatu) na wafanya kazi wengi kwa:-
- Kitengo cha neli (tubemill)
- Kitengo cha kupasua(slitting line)
- Kitengo cha kukata (cut-to-length line)
-
Mafundi umeme wa neli, kupasua na kukata :- wale wenye uzoefu wa miaka 3 watapewa umuhimu

Waendesha kerezo/mashine :- Wale wenye ujuzi wa hali ya juu kuendesha mashine ndiyo wanapaswa kutuma maombi.

Karani wa mapokezi :- Mwombaji awe na muonekano nadhifu, aonge kingereza na Kiswahili kwa ufasaha, mjuzi wa kutumia simu za EPABX na mwenye haiba nzuri

Mafundi umeme (electrician) :- Wawe na shahada au stashahada ya uinjinia katika uhandisi wa umeme na uzoefu wa uendeshaji wa virekebishi vya mitambo

Watunza ghala/ watunza ghala wasaidizi :- Ujuzi wa kompyuta ni lazima pamoja na uzoefu wa miaka 3 mpaka 5 ya utunzaji ghala kwa mtunza ghala na ujuzi na uwezo wa kupanga mali kwa unadhifu kwa wasaidizi wa ghala

Makarani wa kuagiza/kupokea bidhaa :-  Uzoefu wa kazi hii unataiwa watu wenye ujuzi watapewa umuhimu, awe na ujuzi wa kompyuta, uwezo wa kuwakilisha taarifa kwa Kiswahili na kiingereza

Meneja utumishi/ rasilimali watu :- Tunaitaji mwanasheria mwenye uzoefu na aliye na uhusiano wa idara ya serikali inayohusika na sharia, mtaratibu na awezaye kutawala hasira zake

Wahasibu :- wenye uzoefu wa kutaarisha taarifa za mahesabu mwenye uelewa na mitandao tofauti, uelewa wa sharia ya kodi ya thamani (VAT) na sharia zinazohusu malipo. Mwombaji aweze Kiswahili na kingereza kwa ufasaha.

Bwana afya/usalama :- Msiamamizi mwenye uelewa na ufahamu wa maswala ya afya na hali ya usalama (health and safety) katika mazingira hatarishi ya ufanyaji kazi kazini kwa wafanya kazi na maeneo yanayozunguka kiwanda; kuzuia ajali na awe na ufahamu wa kutoa huduma ya kwanza.
Maombi yatumwe yakiambatana na CV pamoja na nakala za vyeti kwa kutumia Email: info@lodhiagroup.com
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Oktoba, 2016

Newer Posts Older Posts
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

LIKE US ON FACEBOOK

© Copyright KaziBongo | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top