OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/43 10 Machi, 2015
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma). Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 34 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei,2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
Nafasi hizi zitajazwa katika ofisi za Wakala wa Vipimo zilizoko Makao Makuu na katika Mikoa yote Tanzania Bara.
Mkaguzi Wa Ndani Mkuu Daraja La I- NAFASI 1 (INARUDIWA)
MAJUKUMU YA KAZI
• Kuidhinisha taarifa ya ukaguzi uliofanyika;
• Kumfahamisha Mtendaji Mkuu kuhusu mabadiliko ya miongozo ya Ukaguzi (Audit guides) na kumshauri kuhusu Mfumo mzuri wa udhibiti wa ndani (Internal Control);
• Kufanya tathmini juu ya ufanisi (effectiveness) katika uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za fedha katika Wakala wa Vipimo;
• Kufanya uchunguzi maalum kuhusu matumizi ya Fedha yasiyofaa (special checks and investigations);
• Kuhakikisha kwamba utendaji kazi na matumizi ya fedha katika Wakala vinazingatia Sheria, Kanuni na taratibu za manunuzi na Kanuni za kimataifa (International Standards);
• Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu ya Wakala kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za fedha na Manunuzi;
• Kumshauri Mtendaji Mkuu kuchukua tahadhari ili kuzuia hasara na matumizi yasiyofaa katika Wakala;
• Kuratibu, kusimamia na kuongoza shughuli za ukaguzi wa ndani.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Shahada ya Biashara au Sanaa ya Uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu (ADA) kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali;
Awe na Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters/Postgraduate Diploma) katika fani ya Uhasibu/Fedha na waliofaulu mtihani wa Taaluma ya Cheti cha Uhasibu (CPA) (T) pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi na mbili (12) katika fani hiyo. Wawe wametoa mchango wa makala/maandiko ya kiuhasibu na Ukaguzi hesabu yanayotambuliwa Kitaifa au Kimataifa watafikiriwa kwanza.
Awe na ujuzi wa kutumia Kompyuta.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7 kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 25 Machi, 2015
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xv. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI KWENYE SEHEMU YA ‘OTHER ATTACHEMENTS’
MKAGUZI WA NDANI MKUU DARAJA LA I (INARUDIWA)
Reviewed by Unknown
on
4:53:00 AM
Rating: