Kumb. Ref. Na
EA.7/96/01/H/41 7 Machi, 2015
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi 80 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.
1.2
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu
shughuli za uhasibu.
·
Kuandika
hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
·
Kutunza
majalada yenye kumbukumbu za hesabu
·
Kupeleka
barua/nyaraka za uhasibu Benki.
·
Kufanya
usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
1.2.1 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa
wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na
NBAA
1.2.2
MSHAHARA
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
1.2.3
MKUFUNZI WA KILIMO MSAIDIZI (AGRICULTURAL TUTOR) – NAFASI
6
1.2.4
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa
mtiririko wa mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans),
·
Kuandaa na kufundisha masomo ya kozi za
astashahada,
·
Kusimamia masomo ya vitendo vya kozi za
stashahada chini ya usimamizi wa mkufunzi mkuu wa somo,
·
Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la
vitendo kwa kozi stashahada,
·
Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo
la vitendo kwa kozi za astashahada,
·
Kupima maendeleo ya wanachuo wa astashahada
kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao na
·
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri
atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.2.5
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita
waliofuzu mafunzo ya Stashahada
|
|
|
(Diploma) ya
Kilimo kutoka MATI au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na
|
|
Serikali.
|
1.2.6
|
MSHAHARA
|
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.
1.2.8
MAJUKUMU YA KAZI
·
Ukadiriaji
wa kodi za ardhi.
1.2.9 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Diploma ya kawaida katika fani ya Usimamizi Ardhi na Uthamini kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka
mitano.
1.2.10 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS C kwa mwezi
1.2.11
FUNDI SANIFU DARAJA II - UPIMAJI NAFASI 3 1.2.12 MAJUKUMU YA KAZI
Sehemu ya Topographic
and Geodetic Survey:
·
Kupanga na kuandaa mahitaji ya kambi za
upimaji, vifaa vya upimaji na mahitaji ya jumla.
1.2.13 SIFA ZA
MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Diploma ya kawaida katika fani ya Upimaji na Ramani, kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka
mitano.
1.2.14 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS C kwa mwezi
1.2.15
MSAIDIZI WA UVUVI – NAFASI 6 1.2.16 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutoa huduma ya ugani kwa wavuvi ikiwa ni
pamoja na matumizi sahihi ya zana za uvuvi na ukuzaji wa viumbe kwenye maji.
·
Kukusanya takwimu na kutunza kumbukumbu za
uvuvi na ukuzaji wa viumbe kwenye maji na kutoa taarifa.
·
Kutoa ushauri kwa vikundi vya ulinzi wa
rasilimali za uvuvi.
·
Kuhakiki
usajili wa vyombo na matumizi ya zana za uvuvi na kutoa taarifa.
·
Kukagua
leseni za uvuvi.
·
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu
wa kitengo zinazohusiana na fani yake.
1.2.17 SIFA ZA
MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV ambao wamepata mafunzo ya uvuvi ya muda wa miaka
miwili na kutunukiwa Astashahada kutoka katika Chuo cha Uvuvi Nyegezi au chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.18 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi.
1.2.19
AFISA NDOROBO MSAIDIZI II (Tsetse Field Officer)- NAFASI
2
1.2.20
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
uchunguzi wa mbung’o na ndorobo katika eneo lake.
·
Kukusanya
takwimu za mbung’o na ndorobo.
·
Kutayarisha
ramani za usambaaji wa mbung’o na ndorobo katika eneo lake.
·
Kupanga
shughuli za uzuiaji mbung’o na ndorobo katika eneo lake.
·
Kuandaa
taarifa za mwezi, nusu na mwaka za uzuiaji wa mbung’o na ndorobo.
·
Kutoa
elimu ya mbinu za uzuiaji wa mbung’o na ndorobo kwa wanavijiji.
·
Kusimamia
shughuli zote za uzuiaji mbung’o na ndorobo katika eneo lake.
·
Kuhamasisha utumiaji wa mbinu salama za
uzuiaji wa mbung’o na ndorobo kwa kuzingatia kanuni ya hifadhi ya mazingira.
·
Kufuatilia taarifa za awali za kuwepo kwa
matukio ya ndorobo (nagana na malale).
·
Atafanya
kazi nyingine zozote za fani yake itakavyoelekezwa na mkuu wake wa
kazi.
1.2.21 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha VI wenye Stashahada katika fani ya Ndorobo na Malisho
kutoka chuo cha Mifugo (MATI au LITI) au chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
1.2.22 MSHAHARA
1.2.23 AFISA USAJILI MSAIDIZI DARAJA LA II (REGISTRATION
ASSISTANT II)-NAFASI 1
1.2.24
MAJUKUMU
YA KAZI
·
Kupokea
na kuingiza kumbukumbu za hati katika kompyuta
·
Kufungua
majalada ya hati mpya
·
Kupokea
maombi na kutayarisha taarifa za uchunguzi wa hati( search report)
·
Kufunga
hati zilizokamilika (binding) na
kuziwasilisha masjala
1.2.25 SIFA ZA
MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye astashahada
ya Sheria (certificate in law), cheti cha Uthamini na Usimamizi wa Ardhi kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
1.2.26 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
1.2.27 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 25 1.2.28
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuendesha magari ya
abiria, magari madogo na malori
·
Kuhakikisha
gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi
wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
·
Kufanya
matengenezo madogo madogo katika gari,
·
Kutunza
na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
1.2.29 SIFA ZA
MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya
uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka
mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la
II.
1.2.30 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
1.2.31 MLINZI
(SECURITY GUARD) – NAFASI 16
·
Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi
inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
·
Kuhahikisha
kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
·
Kulinda
usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
·
Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote
yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
·
Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia
katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
·
Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea
katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika
vyombo vinavyohusika.
·
Kutoa
ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
1.2.33 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato
cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka
katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.34 MSHAHARA
Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
1.2.35
MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 8
1.2.36
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na
ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani,
kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha
vyoo.
·
Kuchukua na kupeleka majalada na hati
nyingine kwa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·
Kusambaza
barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
·
Kutayarisha
chai ya ofisi.
·
Kupeleka
mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
·
Kuhakikisha
kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
·
Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati
wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
·
Kudurufu barua au
machapisho kwenye mashine za kudurufia.
·
Kuweka katika majalada
nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
·
Kutunza vifaa vya ofisi
na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri
katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
1.2.38 MSHAHARA
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA
KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za
kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma,
maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale
waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa
uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na
VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional
certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi
karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na
NECTA).
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 21 Machi,
2015
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
AJIRA UTUMISHI SWAHILI - 7 Machi, 2015
Reviewed by Unknown
on
12:06:00 AM
Rating: