MKUFUNZI DARAJA II (TUTOR GRADE II) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Chuo Cha Ardhi Tabora)
NAFASI 1 - Usimamizi na Uthamini wa Ardhi (Land Management and Valuation) NAFASI 1 - Mipangomiji (Town Planing)
NAFASI 1 - Teknolojia ya Uchapaji (Printing Technology)
53.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha
• Kutoa ushauri kwa wanachuo katika kazi maalum (projects).
• Kusimamia na kuongoza wanachuo katika kazi za darasani na nje.
• Kutoa ushauri wa kiufundi na kitaalam.
• Kuendesha tafiti na ushauri.
• Kuandaa taarifa za tathmini na mapendekezo ya mitaala ya masomo.
53.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani za Mipangomiji (Town Planing), Usimamizi na Uthamini wa Ardhi (Land Management and Valuation) na Teknolojia ya Uchapaji (Printing Technology) kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
53.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
viii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 9 Aprili, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
MKUFUNZI DARAJA II (TUTOR GRADE II)
Reviewed by Unknown
on
11:46:00 PM
Rating: