41.0 AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 3.
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Kigoma/Ujiji.
41.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
• Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Mtaa
• Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa
• Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Mtaa
• Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.
• Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Mtaa
• Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.
• Ataongoza vikao vya maendeleo ya Mtaa vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
• Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
• Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
• Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Mtaa.
• Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika Mtaa.
41.3 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada (Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Atashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
41.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
viii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 9 Aprili, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE III)
Reviewed by Unknown
on
11:53:00 PM
Rating: