TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INATANGAZIA NAFASI ZA KAZI ZA WAKUU WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KATIKA MAJIMBO YOTE YA UCHAGUZI KWA UNGUJA NA PEMBA.
MUOMBAJI WA NAFASI HIYO ANATAKIWA KUWA NA SIFA ZIFUATAZO.
- AWE NI MZANZIBAR.
- AWE NA UMRI USIOPUNGUA MIAKA 30.
- AWE NA ELIMU KWA KIWANGO CHA KIDATO CHA NNE NA KUENDELEA AU UZOEFU WA KAZI YA USIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA USIOPUNGUA CHAGUZI MBILI.
- AWE NA UWEZO WA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
- AWE NA UZOEFU WA KUFANYA DHAMANA ZAKE BILA YA USIMAMIZI
- AWE NA UWEZO WA KUIFAHAMU JAMII YAKE ILIYOMZUNGUUKA.
- AWE NA UWEZO WA KUTEKELEZA SHERIA ZA KIUCHAGUZI.
- AWE NA UWEZO WA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUFANYA HESABU KWA USAHIHI.
- ASIWE NA USHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.
- AWE NA UWEZO WA KUANDIKA RIPOT.
- AWE NA UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHAGUZI.
MUOMBAJI W NAFASI HIZO ATAWAJIBIKA KUAMBATANISHA NAKALA ZA VYETI VYA KUMALIZIA MASOMO KATIKA BARUA YAKE YA MAOMBI.
BARUA ZA MAOMBI ZITUMWE KWA ANUANI IFUATAYO.
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WILAYA,
P.O.BOX 1001,
ZANZIBAR.
WAOMBAJI WOTE WANATAKIWA WAWASILISHE BARUA ZAO ZA MAOMBI KATIKA AFISI ZA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR ZA WILAYA AMBAYO MUOMBAJI ANAOMBA KUFANYIA KAZI HIYO, NA AHAKIKISHE KUWA ANAOMBA KUFANYA KAZI KATIKA JIMBO AMBALO YEYE AKIWA MPIGA KURA ANAWEZA KUITUMIA HAKI YAKE YA KISHERIA YA KUPIGA KURA KWA URAHISI.
PIGA KURA KWA AMANI UPATE MAENDELEO NCHINI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
NAFASI ZA KAZI TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR - 2/13/2016
Reviewed by Unknown
on
12:33:00 AM
Rating: