Kumb. Na EA.7/96/01/G/55 26 Agosti, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL
SECRETARY GRADE III) – NAFASI 11
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuchapa
barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
·
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida
zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
·
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za
matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi
zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
·
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake
majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo
ofisini.
·
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa
kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa
amepewa na wasaidizi hao.
·
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa
Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
·
Kutekeleza
kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
|
|
·
|
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
|
|
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na
|
|
Kiingereza maneno
80 kwa dakika
moja na wawe
wamepata mafunzo ya
|
|
Kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
|
|
katika programu za Window,
Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
|
2.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
Public Service Recruitment
| |
Utumishi wa Umma,
|
Secretariat,
| |
SLP.63100,
|
P.O.Box 63100
| |
Dar es Salaam.
|
Dar es Salaam.
|
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) – NAFASI 11
Reviewed by Unknown
on
12:38:00 AM
Rating: