Kumb.
Na EA.7/96/01/G/55 26
Agosti, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje
na Ushirikiano wa Kimataifa.
AFISA MAMBO YA NJE
DARAJA LA II (SECOND SECRETARY) – NAFASI 10
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa
zinazohusu masuala ya kimahusiano ya kimataifa.
·
Kuhudhuria
mikutano mbalimbali.
·
Kuandaa
mahojiano.
·
Kufuatilia
masuala mbalimbali ya kimataifa.
·
Kufanya
utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
·
Kutunza
kumbukumbu za matukio mbalimbali.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao
wamejiimarisha (major) katika fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations),
Sheria au Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha, wawe wamefanya na kufaulu mtihani
unaotolewa Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.
1.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
na wenye umri usiozidi miaka 45
i.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iii.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo,
nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa
sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
x.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September,
2014
xii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (SECOND SECRETARY) – NAFASI 10
Reviewed by Unknown
on
12:37:00 AM
Rating: