Kumb.
Na EA.7/96/01/H/03 25
Septemba, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma
ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu
la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi 102 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
1.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC)
– NAFASI 25-ZINARUDIWA
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi
wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili
aweze;
·
Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na
kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za kupitisha bomba kwa ajili ya miradi
ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya
inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya maji na usafi wa mazingira ili
kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
·
Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu
kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa
ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa
namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu wa miradi kufanya kazi
yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu wa
miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).
1.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
2.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
2.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya
uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga
pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini
za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuhudumia
uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
·
Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi
ya maji;
2.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).
2.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
1.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya
uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
·
Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili
ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya
aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme,
mota na vifaa vingine umeme vya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili
ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
·
Kuendesha
mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na
ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa
kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
1.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
3.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 2-ZINARUDIWA
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.4
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga
pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini
za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuhudumia
uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
·
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay
a kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi
ya maji;
·
Kumsaidia
Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
1.5
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.
1.6
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
4.0
FUNDI
SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI BOMBA) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN PLUMBING) –
NAFASI 1-INARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.7
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya
kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
·
Kufunga
mitandao ya bomba za aina mbalimbali ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
·
Kufanya usafi na ukaguzi wa mitandao ya bomba
ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
·
Kuwezesha uzalishaji na usambazaji wa maji na
utoaji wa majitaka kwa kupitia mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi nay
a kuzuia uharibifu wa mitandao ya bomba kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa
dharura.
·
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na
kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitandao ya bomba za
miradi ya maji na usafi wa mazingira;
1.8
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja
kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana
Cheti cha ufundi Daraja III (Plumbing).
1.9
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS A kwa mwezi.
5.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER
RESOURCE ENGINEER – NAFASI 14-INARUDIWA
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa
ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji
na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na
matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu
na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi,
uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na
usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
·
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi
na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
·
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa
miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
·
Kutayarisha
bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
·
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji
wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
·
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
5.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya
uhandisi wa Maji (Water Resource
Engineering) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS E kwa mwezi.
6.0
MHANDISI
DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4-INARUDIWA
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
6.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa
ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji
na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na
matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu
na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
·
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi,
uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na
usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
·
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi
na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
·
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa
miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
·
Kutayarisha
bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
·
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji
wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
·
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
6.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya
uhandisi wa Maji (Water Resource with
GIS) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
6.3
MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
yaani TGS E kwa mwezi.
7.0
MHANDISI
KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 6-INARUDIWA
7.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima
kutumia zana za kilimo,
·
Kushiriki katika kufundisha wakulima na
matumizi bora ya zana,
·
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za
umwagiliaji,
·
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya
umwagiliaji,
·
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha
wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
·
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
·
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za
umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
·
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za
za kilimo,
·
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama
kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
·
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora
na
·
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri
waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye shahada ya
kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
Serikali.
7.3 MSHAHARA
·
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani
ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i.
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii.
Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa
Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo,
wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe ipasavyo.
iv.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya
bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi
yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na
vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha
sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa
kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates.
-
Cheti
cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-
Computer
Certificate
-
Vyeti
vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-
Picha
moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix.
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa
katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa
tarehe 30 Novemba 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Oktoba,
2014
xiii.
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono
katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya
Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya
Ajira katika
|
|
Public
Service Recruitment
|
Utumishi wa Umma,
|
|
Secretariat,
|
SLP.63100,
|
|
P.O.Box 63100
|
Dar es Salaam.
|
|
Dar es Salaam.
|
NAFASI ZA AJIRA UTUMISHI - 25 Septemba, 2014
Reviewed by Unknown
on
7:20:00 AM
Rating: