Kumb. Na EA.7/96/01/G/55 26 Agosti, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
3.0
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN
RESOURCES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
3.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote
katika Wizara, Mikoa, Wilaya na Idara zinazojitegemea kulingana na mahali
alipo.
·
Kutafsiri
na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
·
Kutafiti,
kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
·
Kuandaa
na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
·
Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya
mafunzo kwa kushirikiana na vyuo vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
·
Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na
kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
3.2
SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi
Jamii au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
§ Menejimenti
ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
§ Elimu
ya Jamii (Sociologly).
§ Utawala
na Uongozi (Public Administration).
·
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
3.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
Public Service Recruitment
| |
Utumishi wa Umma,
|
Secretariat,
| |
SLP.63100,
|
P.O.Box 63100
| |
Dar es Salaam.
|
Dar es Salaam.
|
AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN RESOURCES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Reviewed by Unknown
on
12:39:00 AM
Rating: