Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba
Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali (MDAs) anatarajia
kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji
kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 1:00 kabla ya muda wa mtihani wa
mchujo kuanza.
2.Usaili utaanza saa moja na nusu asubuhi (1:30) na utafanyika mahali
na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafirian.k
4. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha
nne, sita, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hatimatokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8.Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9.Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth
Certificate)
2
10.Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11.Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba
tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
KUITWA KWENYE USAILI UTAKAOANZA TAREHE 25-29 MEI 2015
KUITWA KWENYE USAILI UTAKAOANZA TAREHE 25-29 MEI 2015
Reviewed by Unknown
on
9:00:00 AM
Rating: