Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
National Food Reserve Agency (NFRA) anatarajia kuendesha usaili na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 4:00 kamili asubuhi kabla ya muda
wa mtihani wa mchujo kuanza.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne,
sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI
RESULTS SLIPS)HAVITAKUBALIWA
5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
6. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
7. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth
Certificate)
8. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
9. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba
tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
10. Wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na
tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo
hili.
USAILI NFRA TAREHE 25-29 MEI 2015(Call for Interview)
USAILI NFRA TAREHE 25-29 MEI 2015 (Call for Interview)
Reviewed by Unknown
on
9:04:00 AM
Rating: