Kuna malalamiko mengi kuhusu matokeo ya admission na inaonekana mengi yanasababishwa na wengi kutofahamu utaratibu.
Kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa Shahada hutolewa na TCU pekeyake. Mfumo huu wa NACTE umeunganishwa na mfumo wa CAS wa TCU utakaotoa majina hayo.
Kabla ya TCU kuyatoa majina hayo, ni lazima kwanza yapite JAC ambayo imefanyika jana. JAC ina jukumu la kuhakikisha hakuna aliyepangiwa chuo zaidi ya kimoja na pia waliochaguliwa wamekidhi viwango.
Majina hayo yalishapelekwa vyuoni wiki iliyopita ili vyuo viyapitie na kuyakubali kabla ya kupita JAC. Hivyo ni kweli vyuo tayari vina majina hayo lakini kiutaratibu havitakiwi kuyatangaza hadi itakapohakikishwa kuwa multiple selections zimeondolewa.
Mara baada ya hapo TCU itaruhusu profiles zenu kuonyesha mlikochaguliwa na vyuo kutangaza.
Mnapaswa kufahamu kuwa vyuo vina mamlaka ya kukataa kupokea baadhi ya wanafunzi kwa sababu mbalimbali.
TAARIFA YA NACTE KWA UMMA - 9/23/2014
Reviewed by Unknown
on
2:11:00 AM
Rating: