AJIRA UTUMISHI - KISWAHILI - 1 Agosti, 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/G/50 1 Agosti, 2014

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 145 za kazi kwa ajili ya Wizara,Idara zinazojitegemea,Wakala,Taasisi za umma na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya


kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

HAVITAKUBALIWA.

viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe19 Agosti, 2014

xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.


1.0 MJIOLOJIA DARAJA LA II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 8

Nafasi

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kupokea na kufuatilia upatikanaji wa taarifa za utafiti wa mistari ya uchungi na mitetemo katika utafutaji wa madini au petroli;

Kukusanya na kuchambua taarifa za mitetemo, mienendo na mabadiliko ya miamba ardhini;

Kutunza kumbukumbu za miamba, madini au petroli;

Kutayarisha rasimu za taarifa za kitaalam na kuziwasilisha kunakohusika;

Kusimamia matumizi ya vifaa vya kitaalam na utunzaji wake; na

Anaweza kuongoza timu ya mafundi sanifu wanapokuwa katika shughuli za utafutaji wa madini au petroli.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika fani ya Jiolojia (pamoja na fani za Jiofizikia au Jiokemia) au sifa nyingine zinazolingana na hizo kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali,

1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

2.0 MHANDISI MIGODI DARAJA LA II – (MINING ENGINEER)- NAFASI 14

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya kazi chini ya uangalizi wa mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya Usajili wa Wahandisi kama “Professional Engineer” ili kupata uzoefu unaotakiwa.

Kufanya kazi kwa vitendo katika fanii zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

Kuwaelimisha wachimbaji wadogo kuhusu sheria, kanuni na masuala ya kitaalamu ya uchimbaji, uchenguaji na masoko ya madini.

Kupitia taarifa za kila mwezi za ofisi za madini.

Kukusanya na kuchambua taarifa na takwimu za uchimbaji madini.

Kutunza kumbukumbu za usafirishaji, utangazaji biashara na matumizi ya baruti.

2.2 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

3.0 MCHAMBUZI MIFUMO YA KOMPYUTA DARAJA LA II – NAFASI 13

Nafasi

3.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuweka kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.

Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na uthibiti unaohusu Kompyuta.

Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara/Idara/Vituo mbalimbali vya kazi.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

3.3 MSHAHARA
•  Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.


4.0 MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) – NAFASI 11

Nafasi

4.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya  na kuratibu takwimu

Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)

Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati au sifa zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia Kompyuta.

4.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

5.0 NAHODHA DARAJA LA II – (SKIPPER GRADE II) – NAFASI 1

Nafasi

5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kubuni na kuunda zana za kuvulia samaki (Fishing Gears).

Kutunza na kutengeneza zana za kuvulia samaki.

Kuongoza na kuendesha meli/boti ndogo za futi 40 zenye uzito wa kuandikishwa wa tani 50-200 (GRT).

Kuendesha shughuli za uvuvi katika meli/boti.

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Unahodha na Uvuvi (Master Fisherman) kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

5.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi.


6.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MIGODI (MINING TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 14

6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua na kupima viwanja kwa ajili ya waombaji wadogo wadogo

Kusimamia wapimaji na kuhakikisha wanapima kwa kiwango kinachotakiwa

Kuandaa “action plan” na kuhakikisha inafuatwa

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:

Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani migodi

Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za migodi

Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi migodi kutika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

7.1 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1

7.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.

7.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

7.3  MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa mwezi.

8.1 MKUTUBI DARAJA LA II – NAFASI 1

8.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuratibu shughuli za ukuzaji wa utamaduni kitaifa.

Kuratibu na kusimamia shughuli za ukaguzi na udhibiti maonyesho ya filamu na video katika ngazi ya taifa.

Kushauri juu ya mitaala ya mafunzo na elimu ya fani za utamaduni.

Kusimamia usajili wa vikundi na vyama vya fani za utamaduni.

Kushauri juu ya ujenzi wa majukwaa na majumba ya utamaduni yenye hadhi ya kitaifa.

Kuratibu shughuli za utafiti wa mila na desturi nchini.

Kusimamia na kuratibu ukuzaji wa matumizi fasaha na sanifu ya Kiswahili nchini.

Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.

8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya ukutubi au sifa inayolingana na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

9.1 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NYARAKA) – NAFASI 50 9.1 MAJUKUMU YA KAZI

Daraja hili ni la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Wasaidizi wa Kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la I

Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.

Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.

Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.

Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.

Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.

9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi

10.0 MSAIDIZI UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II - NAFASI 3

10.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia manzuki.

Kutunza hifadhi za nyuki.

Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki.

Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti.

Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo.

Kutoa leseni za biashara ya mazao ya nyuki.

Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki.

Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.

10.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Ufugaji Nyuki kutoka katika vyyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

10.3 MSHAHARA

• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B

11.0  MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - (GARDNER II) NAFASI 3

Nafasi

11.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kupanda mboga, matunda, n.k. katika bustani.

Kupalilia mazao katika bustani.

Kupanda maua katika maeneo yanayohusika.

Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji.

Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.

11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti katika fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na

upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu.

11.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.

12.0  MWANDAZI DARAJA LA II (WAITER GRADE II) - NAFASI 1

Nafasi

12.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa meza ya kulia chakula.

Kupamba meza ya kulia chakula

Kupanga vifaa vya kulia chakula mezani.

Kuondoa vyombo baada ya kula chakula

12.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu mafunzo si chini ya mwaka mmoja katika fani ya ‘Food and Bevarages’ yatolewayo na vyuo vya

Forodhani Dar es Salaam. Masoka Moshi, Arusha Hotel na Y.M.C.A ya Moshi na Vyuo vingine vinavyolingana ambavyo vitatambuliwa na Serikali.

12.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi.

13.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 26

13.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.

Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.

Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu

Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.

Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.

13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA

13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi

14.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI UPIMAJI NA RAMANI (MAPPING/CARTOGRAPHER ASSISTANT) – NAFASI 1

14.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutayarisha alama za upimaji (survey pillars, becons etc).

Kufanya kazi za upimaji zisizohitaji ujuzi (semi skilled tasks).

Kutunza kumbukumbu za ramani zinazotayarishwa.

Kuchora michoro ya upimaji (survey plan)

14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita wenye mchepuo wa mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Upimaji na Ramani, Usimamizi Ardhi, Uthamini na Usajili katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

14.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi.

AJIRA UTUMISHI - KISWAHILI - 1 Agosti, 2014 AJIRA UTUMISHI - KISWAHILI - 1 Agosti, 2014 Reviewed by Unknown on 12:12:00 PM Rating: 5

JOBS CATEGORY

Tanzania Kenya NGO JOBS Uganda Best Jobs Consultancy Rwanda ICT JOBS Administrative United Nations Sudan Best Jobs Finance Health - Medical Engineering Ethiopia Education Agricultural Lecturer Human Resources Somalia Media Congo - Kinshasa Legal Jobs Bank Jobs Monitoring and Evaluation Mining World Vision Burundi Procurement African Barrick Gold Accountant Zambia Sales and Marketing US EMBASSY East African Community Mozambique Telecoms Research CARE International Save The Children Plan International Arusha Malawi South Sudan Oxfam Scholarships African Development Bank Finance and Administration SafariCom Aviation The Commonwealth American Embassy Sales Zanzibar Environmental Catholic Relief Services Dar es salaam USAID Operations FHI 360 UNDP Security World Bank Economist TradeMark East Africa Unicef Hospitality Managers International Rescue Committee (IRC) Restless Development Accounting Civil Engineers AMREF Morogoro Utumishi AfDB African Development Bank COOPI - Cooperazione Internazionale Driver - Logistics Path International Mwanza African Union Tigo Jobs Marketing Mbeya Teaching Au African Union PSI Population Services International Pwc PricewaterhouseCoopers East African Breweries North Mara Gold Mine ACTED Djibouti Malaria Consortium Bulyanhulu Gold Mine DFID Driver Buzwagi Gold Mine Jhpiego COMESA FINCA JOBS International Jobs Adeso Danish Refugee Council Kilimanjaro Nairobi Coca-Cola Handicap International Pact International Rio Tinto Solidarités International Tender EGPAF Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation Logistics Serengeti Breweries Ltd Nation Media Group Africare Norwegian Refugee Council Samaritan's Purse Chemonics International COUNTRY DIRECTOR ICAP of Columbia University InterShips Precision Air RwandAir Marie Stopes International (MSI) Serengeti Breweries Volunteer Climate Change IGAD Tetra Tech ARD Agriculture Jobs Dodoma Iringa One Acre Fund Project Management Clinton Health Access Initiative (CHAI Technoserve Twaweza East Africa ActionAid Lutheran World Federation SADC Secretariat Tanga Vso International ACDI/VOCA Halmashauri Agha Khan Kenya Commercial Bank World Agroforestry Centre Deloitte East Africa International Organization for Migration (IOM) COMESA Secretariat: Software Engineering Safety and Security Shinyanga Jobs Tanzania Breweries Pathfinder International World Health Organization KPMG TANROADS Tanzania Electric Supply Company British Council Futures Group KCB BANK UN-Habitat WFP World Food Programme Barclays GEITA GOLD MINING TANESCO Electrical Engineer Food and Agriculture Organization GOAL Mombasa Tabora WWF World Wide Fund for Nature Microsoft Tanzania Ports Authority East African Development Bank Family Health International (FHI) IBM EAST AFRICA IntraHealth International Mercy Corps SERIKALINI - GOVERNMENT OF TANZANIA AccessBank Community Development Jobs Data Base Management Google Africa ICAP - TZ KEMRI/CDC Program WaterAid Tanzania Auditor SNV International Stanbic Bank Amnesty Horn Relief Kampala Management Systems International (MSI) Standard Chartered Bank VETA Christian Aid DIAMOND TRUST BANK Helen Keller International Help Age Mtwara Uganda Telecom Airtel Africa Equity Bank Internships Marie Stopes TCRA Web Development B B C WORLD SERVICE Human Rights Kigali Makerere University Nile Basin Initiative Kenyatta University Kigoma Mzumbe University NSSF National Social Security Fund Nile Breweries Limited Tulawaka Gold Mine University of Nairobi kenya Airways Bank of Tanzania Graduates MTN Muhimbili National Hospital Nepad Partners in Health Room to Read SUMATRA UNWOMEN African Wildlife foundation (AWF) KEMRI Kagera Librarian MENTOR Initiative Trainee USAILI - INTERVIEW Uiversity of Nairobi WaterAid International icipe Project CAFOD - Catholic Agency for Overseas Development Egerton University EngenderHealth Goal Ireland Kenyan Banks Lake Victoria Basin Commission Peace Corps TANAPA TASAF Tanzania Social Action Fund Zanzibar University ACB AKIBA COMMERCIAL BANK AGRA Alliance for a Green Revolution in Africa Advans Bank Ethiopian Airlines Freedom House IITA International Institute of Tropical Agriculture Legal Moshi NMB BANK Resolute Tanzania Singida Uganda Uganda National Roads Authority University of Dar es salaam University of Dodoma British High Commission ChildFund EWURA FilmAid International NECTA TPDC Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) United States International University World Concern Aga Khan Foundation CBA Commercial Bank of Africa Ecomist Ernst and Young IUCN International Union for Conservation of Nature International Medical Corps Islamic Relief Kakira Sugar Musoma National Institute for Medical Research OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA Relief International TAA Tanzania Airports Authority Trócaire Uganda Revenue Authority VODACOM TANZANIA VSF Belgium Architects Hivos IFC International Finance Corporation Ifakara Health Institute Inoorero University International Commercial Bank Kenya Red Cross Society MADEREVA Medical Oil and Gas Pwani University College SOKOINE UNIVERSITY Tumaini University Water Engineering AWF African Wildlife Foundation Acacia Mining Accounts African Virtual University Altima Africa Ardhi University Bank of Uganda Business Development Concultancy Del Monte Kenya Embassies Kenya Airports Authority Lake Victoria South Water Services Board Mara National Bank of Commerce RECORDS MANAGEMENT JOBS RUKWA Ruvuma Search for Common Ground Songea TTCL Tanzania Telecommunications Company Limited Unilever War Child International Zinduka Afrika ACORD AKU ​Aga Khan University Africa Nazarene University Africa Rice Center (AfricaRice) Aga Khan Health Services CRDB BANK Commercial Bank of Africa Daraja Tanzania Engineers Registration Board (ERB) Fina Bank International Potato Center International Potato Center (CIP) Intrahealth Jomo Kenyatta University Kilimanjaro Christian Medical Centre Kyambogo University Lindi Jobs MCL Mwananchi Communications MUHAS-harvad Moi University NBC BANK National University of Rwanda Ngorongoro Conservation Area Authority Njombe Nuru International Nzoia sugar Company RTI International SUA SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE THE LAW SCHOOL OF TANZANIA TRA Tanzania Revenue Authority Tanzania Postal Bank The Foundation For Civil Society Udhamini wa Masomo Western Union AIR TANZANIA Action Against Hunger (ACF) Agricultural Society of Kenya BRALIRWA Bondo University College Caritas Comoros Concern Worldwide Conservation Jobs Consolidated Bank of Kenya DHL Express Ewaso Ngiro South River Basin Development Authority Geologist Gulf African Bank INSTITUTE OF ADULT EDUCATION Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology Kabale University Kabale University (KAB) Kenya Ports Authority KickStart International MORUWASA Morogoro Urban Water and Sanitation Authority MSH Management Sciences for Health Mumias Sugar Company Nairobi Hospital Nkumba University Rural Electrification Agency SOKINE UNIVERSITY SONGWE STAMIGOLD Stores TACAIDS TARURA TCU Tanzania Commission for Universities Tullow Oil World Lung Foundation (WLF) ALAF Limited Aga Khan Development Network (AKDN) Aga Khan Hospital Air Malawi American Refuge Committee BENKI YA POSTA - TPB BANK BTC Belgian Technical Cooperation Bhttp://www.blogger.com/img/blank.gifank of Tanzania Bioversity International CHF International Customer Service Jobs DANGOTE DIT DAR ES SALAAM INSTITUTE OF TECHNOLOGY Danida Dar es Salaam Institute of Technology Daystar University ECOBANK ETDCO Electrical Transmission and Distribution Construction and Maintenance Company European Union IFM INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT INSURANCE JOBS - BIMA ITECH Internews® Network KUITWA KAZINI Kenya Accreditation Service Kenya Polytechnic University College Kilombero Sugar Company Kisii University College Kisumu Laboratory Jobs MSD MEDICAL STORES DEPARTMENT MSF Switzerland Management Sciences for Health Manyara Maseno University Ministry of State for Planning Muteesa 1 Royal University Médecins Sans Frontières NIDA National Identification Authority Narok University College OSHA Occupational safety and Health Authority Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA) PA PAC PEPSI POLICE - POLISI Petroleum EngineerS RWANDA HOUSING AUTHORITY Seychelles Songas TBC TANZANIA BROADCASTING CORPORATION TBS TANZANIA BUREAU OF STANDARDS TFDA TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY TIB - Tanzania Investment Bank Tanzania Mortagage Refinance Company Tanzania Teachers’ Union Transmara Sugar Company Tropical Pesticides Research Institute Tumba College of Technology Twiga Cement UNESCO UNOCHA Umma University University WRP Walter Reed Project ZANTEL ao uga
Powered by Blogger.