TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
1.0 tume ya utumishi wa mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama na. 4/2011 tume ya utumish wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbali mbali wa mahakama.
1.1 hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasiya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika ofisi za mahakama ya Tanzania ambazo ziko katika mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
2.0 AFISA UTUMISHI II AFISA TAWALA II (TGS D)
waombaji watapangiwa katika mahakama kuu (T) na mahakama za mikoa
2.1 AFISA UTUMISHI II
2.1.1SIFA
shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii au sanaa katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na na serikali ambao wamejiimarisa (Major) katika kimojawapo ya fani
i. Maliasili ya rasilimali watu (humani resourse management)
ii. Elimu ya jamii(sociology)
iii. Utawala na uongozi (public adimistration)
iv. Mipango ya utumishi wa (man power planning)
v. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta
2.1.2 kazi za afisa utumishi Daraja la II
i. kutunza kumbukumbu sahiji za utumishi wote
ii. kutafsiri na kushughurikia utekerezaji wa miundo ya utumishi.
iii. kutafiti, kuchambua na kupanga takimuna kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya utumishi
iv. kushughurikia masuala mbalimbali ya kila siku.
2.2 AFISA TAWALA II TGS D Nafasi 6.
2.2.1 Shahada ya kwaza kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikali katika fasi zifuatazo.
i. utawala, elimu ya jamii ,sharia ( mwenye cheti cha Law school) menejiment umma, uchumi na mwenye ujuzi wa kompyuta.
2.2.2 kazi za maafisa tawala
i. kuweka kumbukumbu za matkio mhimu
ii. kusimamia utekerezaji wa sharia, sera, kanuni na taratibu mbali mbali
iii. kusimamia kazi za tawala na uendeshaji
3.0 mwisho wa kupokea maombi barua za maombihayo ni tar 11/8/2014 saa 9 30 alasiri
4.0. barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombak=ji na kuambatanisha
- vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo
-vifupicho wa taarifa za mwombaji (cv)
-kivuli cha cheti cha kuzaliwa
-picha mbili (passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa umma wanapaswa kupitihsa maombi yoa kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa umma.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa
katibu
tume ya utumishi wa mahakama ya Tanzania
SLP. 8391,
DAR ES SALAAM
KATIBU
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA
SLP. 8391,
DAR ES SALAAM
TANZANIA.
AJIRA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA - 8/4/2014
Reviewed by Unknown
on
11:09:00 AM
Rating: