Kumb. Na EA.7/96/01/G/55 26 Agosti, 2014
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
5.0
MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
5.1
MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na
ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani,
kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha
vyoo.
·
Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine
kwa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
·
Kusambaza
barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
·
Kutayarisha
chai ya ofisi.
·
Kupeleka
mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
·
Kuhakikisha
kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
·
Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati
wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
5
·
Kuweka
katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
·
Kutunza
vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
5.2
|
SIFA ZA MWOMBAJI
|
·
|
Kuajiriwa wahitimu
wa kidato cha
nne waliofaulu vizuri
katika masomo ya
|
|
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
|
5.3
|
MSHAHARA
|
·
Kwa
kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
Public Service Recruitment
| |
Utumishi wa Umma,
|
Secretariat,
| |
SLP.63100,
|
P.O.Box 63100
| |
Dar es Salaam.
|
Dar es Salaam.
|
MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 5
Reviewed by Unknown
on
12:40:00 AM
Rating: