Mtendaji wa Mtaa - Halmashauri ya Manispaa ya Tabora

Mtendaji wa Mtaa daraja la III Ngazi ya Mshahara TGS B nafasi (97)

Sifa zinazotakiwa
Awe na elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI)
Aliyehitimu mafunzo yo Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo, Utawala, Sheria, Elimu ya jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya jamii na sayansi ya sanaa kutoka cha Serikali za mitaa Dodoma au Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi atakazofanya
Afisa Masuuli na mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa Kusimamia ulinzi na usalama wa Raia na mali zao
Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mitaa
Katibu wa mikutano wa kamati zote za Halmashauri ya Mtaa Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za mtaa.
APPLICATION INSTRUCTIONS:

Utaratibu wa Kuomba:
Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi katika sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Waombaji watakaoitwa kwenye usaili waje na vyeti halisi (Original Certificate)
Barua za maombi ziambatane na maelezo binafsi ya mwombaji (CV)
Barua za maombi ziambatanishwe no nakala za vyetivya Elimu, Taaluma,cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (passport size)
Waombaji wanatakiwa wawe na umri kuanzia miaka 18 usiozidi 45.
Waombaji waandike namba za simu na anuani zao katiko barua yo maombi ..
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30/08/2015. Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
S.LP 174, TABORA.
Sipara Liana Mkurugenzi wa Manispaa Tabora
Mtendaji wa Mtaa - Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mtendaji wa Mtaa - Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Reviewed by Unknown on 3:14:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.