BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na 27 ya mwaka 1967.
63.1 MHASIBU MKUU DARAJA II
66.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuratibu kazi ya kujibu hoja za ukaguzi.
· Kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.
· Kuandaa na kuoanisha taarifa za mwezi za Benki.
· Kuandaa taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka.
· Kusimamia, kuthibitisha na kuidhinisha malipo.
· Kufanya kazi zingine kama atakavyoagizwa na msimamizi wake wa kazi.
66.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili ya Uhasibu/ Biashara yenye mwelekeo wa Uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
· Awe na CPA (T).
· Mwenye uwezo wa kutumia mifumo ya kompyuta ya kiuhasibu.
· Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) mfululizo katika fani ya uhasibu.
66.1.3 MSHAHARA - PGSS 17
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
viii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
MHASIBU MKUU DARAJA II
Reviewed by Unknown
on
11:38:00 PM
Rating: