Loading...

FUNDI SANIFU DARAJA LA II - UFUNDI NA UMEME (TECHNICIAN GRADE II MECHANICS & ELECTRICAL)


43.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - UFUNDI NA UMEME (TECHNICIAN GRADE II MECHANICS & ELECTRICAL) – NAFASI 12

Nafasi hizi ni kwa ajili ya, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Kishapu Halamshauri za Manispaa ya Morogoro na Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.


43.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.

Kufanya upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.

Kufanya kazi za kutengeneza   mitambo, magari,na vifaa vya Umeme

Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme

Kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na Umeme.

43.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:

Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.

Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,

Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

43.4 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)

watatu wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

viii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.

x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.

xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 9 Aprili, 2013

xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.

Newer Posts Older Posts
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

LIKE US ON FACEBOOK

© Copyright KaziBongo | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top