60.0 FUNDISANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
60.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
• Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
• Kufanya kazi za upimaji ( Survey ) wa barabara,majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa,
60.3 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa Ujenzi kutoka katika chuo
kinachotambuliwa na serikali,
Au
• Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II kutoka chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani ya ufundi wa Ujenzi.
60.4 MSHAHARA -- TGS A
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
viii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 9 Aprili, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
FUNDI SANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN )
Reviewed by Unknown
on
11:40:00 PM
Rating: