Loading...

Nafasi za Kazi Kagera, Shinyanga, Geita and Mara

Je unataka kuendesha maisha yako mwenyewe? ZOLA inakupatia fursa hiyo.
Mwezi uliopita, Wakala wetu wa Mauzo alifanikiwa kupata zaidi ya shilingi milioni 2, wewe pia unaweza kufanikiwa hivyo.Tutakupatia mafunzo, unachohitaji ni kua na tabia nzuri, uwezo wa kujifunza haraka na moyo wa kujituma.

Off.Grid:Electric ni kampuni inayokua kwa kasi, inatoa huduma za umeme kwa gharama nafuu na za kuaminika katika maeneo yanayokosa huduma hizo. Kampuni inatumia nishati mbadala kutoa huduma ya umeme wa muda mrefu kwa wateja ambao wameathirika kutokana na huduma ghali na isiyokua ya uhakika, au hawajafikiwa kabisa na huduma ya umeme. Makao makuu ya kampuni yako Arusha Tanzania.

Mpaka sasa Zola imetoa huduma ya umeme wa jua kwa zaidi ya kaya laki moja nchini Tanzania.

Jiunge na Timu ya Zola:
Kwa sasa, tunatafuta wajasiriamali wanaotaka fursa ya kuimarisha biashara na kubadilisha maisha yao.

Tunatafuta watu wa kujiunga na timu yetu ya mauzo kama mawakala kwenye maeneo yafuatayo;

•Kagera:Ngara, Muleba, Kyerwa, Karagwe.
•Shinyanga:Kahama Mjini, Kahama Vijijini.
•Geita:
•Mara:Rorya,Butiama,Serengeti

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya maombi;
•Uwe unaishi au uwe tayari kuishi kwenye wilaya au kata uliyochaguliwa.
•Uwe na elimu ya kuanzia form four na kuendelea.
•Uwe na umri kati ya miaka 18-35.
•Ni lazima ujue Kusoma na Kuandika.
•Ukifanikiwa kupita kwenye usahili, utaajiriwa kama Wakala mauzo.
•Wakala ambaye atakua na idadi kubwa ya mauzo kwa miezi mitatu mfululizo,atapata nafasi ya kuajiliwa kama mfanyakazi wa kudumu,atalipwa mshahara wa awali pamoja na mafao mengine kama fao la matibabu na mfuko wa jamii.
•Ukishathibitishwa kua wakala wa mauzo,utaitajika kuwa na shillingi 200,000/- itakayo kuwezesha kununua simu pamoja na salio la Zola.
•Uwe na account ya m-pesa.

Hatua zifuatazo zitafanyika wakati wa usahili ili kupata wafanyakazi sahihi
•Usahili kwa njia ya simu; hii itafanyika kwa watu wote watakaokua wamejisajili kwa njia ya mtandao au simu.
•Usahili wa ana kwa ana; huu utafanyika kwa wale watakaokua wamepita usahili kwa njia ya simu.
•Wiki moja na nusu ya mafunzo ya mauzo; hii itakua kwa wale wote waliopita usahili wa ana kwa ana.

Ili ufanikiwe kwenye mambo yaliyotajwa hapo juu, tafadhali fuatilia hatua zifuatazo:

•kopi anuani hii https://goo.gl/Llofzq kwenye kisakuzi (browser) cha kompyuta yako na kisha ujaze form.

•Mwisho wa kujaza form hii ni tarehe 6/11/2016. Hatutapokea maombi yatakayochelewa.

•Iwapo utashindwa kujisajili mwenyewe, lakini bado unahitaji kazi hii, tuma SMS kwenda 0769 046216 ikiwa na ujumbe ufuatao “Majina yako mawili,mkoa,wilaya na kata unayotokea, namba ya simu, pamoja na umri.”

Baada ya kumaliza usajili, mwakilishi kutoka idara ya rasilimali watu atakujulisha utaratibu utakaofatia.

Application Instructions

Ili ufanikiwe kwenye mambo yaliyotajwa hapo juu, tafadhali fuatilia hatua zifuatazo:
•Kopi anuani hii https://goo.gl/Llofzq kwenye kisakuzi (browser) cha kompyuta yako na kisha ujaze form.
•Mwisho wa kujaza form hii ni tarehe 15/11/2016. Hatutapokea maombi yatakayochelewa.
•Iwapo utashindwa kujisajili mwenyewe, lakini bado unahitaji kazi hii, tuma SMS kwenda 0769 046216 ikiwa na ujumbe ufuatao “Majina yako mawili,mkoa,wilaya na kata unayotokea, namba ya simu, pamoja na umri.”
Newer Posts Older Posts
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

LIKE US ON FACEBOOK

© Copyright KaziBongo | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top