Kuitwa kwenye USAILI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
Chuo Cha Ufundi Arusha kinatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwaajiri waombaji watakaofaulu usaili kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. Kuja na vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji
2. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
3. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
4. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa.
5. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
6. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
7. Wale ambao walisoma nje ya Nchi wahakikishe kuwa vyeti vyao vinapata ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
8. Wale ambao wana Ajira rasmi waje na barua za ruhusa kutoka kwa waajiri wao.
9. Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya Chuo: - ARUSHA TECHNICAL COLLEGE : Skills make the difference
Chuo Cha Ufundi Arusha kinawatangazia wafuatao kuwa wanahitajika kwenye usaili kwa nafasi walizoomba ambazo zilitangazwa tarehe 30 Machi 2015 na tarehe 18 Juni 2015. Usaili utafanyika Chuo cha Ufundi Arusha tarehe 21 na 22 Septemba, 2015 saa mbili Asubuhi. Aidha tarehe ya usaili kwa kila nafasi imeainishwa hivyo wasailiwa wote mnaombwa kuzingatia tarehe husika.
KWA MAELEZO ZAIDI PAKUA TANGAZO HILO HAPO CHINI
Kuitwa kwenye USAILI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
Reviewed by Unknown
on
12:02:00 PM
Rating: 5