Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imepanga kuajiri
Wataalam wa Kada za Mifugo na Uvuvi katika mwaka 2012/2013. Hivyo, tunapenda kuwatangazia
Watanzania wote wenye sifa watume barua za maombi ya kazi zifuatazo:
1. Daktari Mifugo Mkufunzi Daraja la II (Veterinary Tutor II) Nafasi 1
(a) Sifa za
waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Tiba ya
Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo Tanzania.
(b) Majukumu
- Kutafsiri
mihutasari ya mafunzo kwenye masomo;
- Kuandaa
mtiririko wa kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadharia na vitendo;
- Kufundisha kozi
za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na vitendo;
- Kuandaa na
kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza;
- Kupima
maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinaehohusika na
kutunza alama zao;
- Kupima
maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na madaktari/maofisa mifugo wa
wilaya, viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).
(c) Mshahara
wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS F
2.
Daktari Utafiti Mifugo Daraja la II (Veterinary Research Officer II)
Nafasi 2
(a) Sifa za
waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa
Mifugo Tanzania.
(b) Majukumu
- Kujifunza na
kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa afya na maradhi ya mifugo;
- Kuweka
kumbukumbu za utafiti;
- Kusaidia
kuendesha semina za maonyesho ya ufugaji bora;
- Kuandaa
mapendekezo ya Utafiti (Reserach
Proposal) kwa kushirikiana na Daktari Utafiti Mifugo anayemsimamia;
- Kufanya utafiti chini ya
usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi;
- Kukusanya na kuchambua takwimu
za utafiti unaoendelea na;
- Kuchapisha taarifa na makala
za Utafiti.
(c) Mshahara wa watumishi wa Serikali ngazi ya
TGRS C
3. Afisa Utafiti Mifugo
Daraja la II (Livestock Research Officer
II) Nafasi 5
(a) Sifa za
waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu
cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
(b) Majukumu
- Kujifunza na kumudu mbinu na
taratibu za utafiti wa mifugo/ndorobo.
- Kufanya utafiti chini ya
usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
- Kuandika na Kuweka kumbukumbu
za utafiti.
- Kusaidia kuendesha semina na
maonyesho ya ufugaji bora.
- Kuandaa mapendekezo ya utafiti
(Research Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo
anayemsimamia.
- Kufanya kazi zo zote kama
atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi
Mshahara wa watumishi
wa Serikali ngazi ya TGRS A
4. Mkufunzi Mifugo Daraja
la II (Livestock Tutor II) Nafasi
1
(a) Sifa za
waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Mifugo au Elimu, Mafunzo
na Ugani kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kutafsiri mihutasari ya
mafunzo kwenye masomo.
- Kuandaa mtiririko wa kila somo
(lesson plan) kwa upande wa nadharia na vitendo.
- Kufundisha kozi za stashahada
na astashahada kwa upande wa nadharia na vitendo.
- Kuandaa na kupanga somo la
vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
- Kupima maendeleo ya wanachuo
kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
- Kupima maendeleo ya wanachuo
kwa kushirikiana na maofisa mifugo wa wilaya, viwandani wakati wa mafunzo
kwa vitendo (Field Practicals).
Mshahara wa watumishi
wa Serikali ngazi ya TGS D
5. Afisa Mifugo Msaidizi
Daraja la II (Livestock Field Officer II) Nafasi 16
(a) Sifa za waombaji `
Waombaji wawe wamehitimu Elimu ya kidato cha IV au cha VI wenye Stashahada
(Diploma) ya Mifugo kutoka vyuo vya Mifugo (Livestock Training Institute –
LITI) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kufanya
uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake;
- Kukusanya
takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na kuandika
ripoti;
- Kushirikiana na
Wakaguzi wa Afya, kukagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara;
- Kutibu na kutoa
chanjo za magonjwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa Mifugo na
kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa;
- Kusimamia
uchanganyaji wa dawa ya josho;
- Kushauri
wafugaji juu ya mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa ndama;
- Kusaidia katika
uhamilishaji (Artificial Insermination) na Uzalishaji (Breeding) wa mifugo
kwa ujumla;
- Kukusanya
takwimu za maendeleo ya mifugo katika eneo lake na;
- Kushauri na
kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundombinu
inayohusiana na ufugaji bora.
( c ) Mshahara
wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS C
6. Mhandisi Baharini II (Marine Engineer II) Nafasi 1
(a) Sifa za
waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka
Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kusimamia
ufungaji wa mitambo katika vyombo vya uvuvi;
- Kushauri
juu ya aina za vyombo/mitambo inayostahili kuendeleza uvuvi;
- Kusimamia
matengenezo ya vyombo vya uvuvi na;
- Kusimamia
uendeshaji wa mitambo ya vyombo vya baharini.
(c ) Mshahara
wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS E
7. Mkunfuzi wa Mifugo
Msaidizi Daraja la II (Assistant Livestock Tutor II) Nafasi 1
(a) Sifa za waombaji `
Waombaji wawe wamehitimu Elimu ya kidato cha IV au cha VI wenye Stashahada
(Diploma) ya Mifugo kutoka vyuo vya Mifugo (Livestock Training Institute –
LITI) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kuandaa
mtiririko (Lesson Plan) wa somo;
- Kufundisha Kozi
ya Astashahada ya Mifugo kwa Wanafunzi na wafugaji;
- Kusimamia masomo ya vitendo chini ya usimamizi wa
Mkufunzi Mkuu wa somo;
- Kuandaa na
kupanaga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo;
- Kuwapima
wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo na
- Anaweza kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Kitengo (Dairy,Poultly,maabara, museum)
( c ) Mshahara wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS C
8. Fundi Sanifu
Maabara za Mifugo Daraja la II
(Veterinary Laboratory Technician II)
Nafasi 2
(a) Sifa za waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Elimu ya kidato cha VI wenye Stashahada
(Diploma) katika fani ya Fundi Sanifu Maabara (Mifugo) kutoka Chuo cha Mifugo
(LITI) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kukusanya
sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara;
- Kuwasaidia wataalam
kuandaa vifaa vya uchunguzi;
- Kutunza takwimu
za uchunguzi;
- Kutunza usafi wa maabara na
vyombo vilivyomo;
( c ) Mshahara
wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS C
9. Afisa Uvuvi Msaidizi II (Asistant Fisheries
Officer II) Nafasi 2
(a) Sifa za waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Elimu ya kidato cha VI wenye Stashahada
(Diploma) Uvuvi
au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing) kutoka vyuo
vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi, Nyegezi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kutengeneza,
Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvL
- Kutunza na
kuangalia mabwawa ya samaki
- Kutega mitego
Ziwani au Baharini.
- Kutengeneza
nyavu ndogo ndogo.
- Kuwapa chakula
samaki katika mabwawa.
- Kuvua samaki
katika mabwawa.
- Kutoa ushauri
kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi.
- Kukusanya
takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki.
- Kutoa ushauri
juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao
yatokanayo na samaki.
- Kuwaelimisha
wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu I
( c ) Mshahara
wa watumishi wa Serikali ngazi ya TGS C
10.
Mteknolojia wa
Samaki II (Fish Technologist II) Nafasi
1
(a) Sifa za waombaji
Waombaji wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi
ya Chakula (Food Science and Food Nutrition, Food Technology, Microbiology)
kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
(b) Majukumu
- Kutoa
ushauri juu ya utayarishaji, utengenezaji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki
na mazao yatokanayo na uvuvi;
- Kusimamia
na kushauri juu ya Kanuni za uthibiti ubora wa Samaki na mazao yake;
- Kutoa
ushauri juu ya matumizi mbalimbali ya samaki kama chakula bora katika
viwanda na maeneo mengine;
- Kudhibiti
ubora wa samaki katika mialo;
- Kuthibiti
usafi katika maeneo ya kupokelea samaki na;
- Kukagua
nyaraka mbalimbali zinazotakiwa kutunzwa melini na viwandani.
(c ) Mshahara wa watumishi wa Serikali
ngazi ya TGS D
MAMBO YA KUZINGATIA
(i)
Barua za maombi
zimbatane na Maelezo Binafsi (CV), picha
ndogo za 2 ukubwa wa pasipoti, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu elimu ya
Sekondari na Shahada;
(ii)
Waombaji wawe na
umri usiozidi miaka 45;
(iii)
Wahitimu
walioajiriwa Serikalini hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi kwa sababu tayari wana
ajira;
(iv)
Wahitimu waliotuma
maombi yao kabla ya tangazo hili wanashauriwa kutuma maombi upya;
(v)
Barua zote za maombi
ziwasilishwe katika muda wa siku saba kuanzia tarehe ya kwanza ya kutolewa
tangazo hili;
(vi)
Tangazo hili
linapatikana kwenye Tovuti ya Wizara www.mifugouvuvi.go.tz
na;
(vii)
Barua zote zitumwe
kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
S.L.P 9152,
DAR ES SALAAM.
NAFASI ZA KAZI MIFUGO NA UVUVI JULAI 2013
Reviewed by Unknown
on
6:26:00 AM
Rating: