The Occupational Safety and Health Authority (OSHA) is the government agency under the Prime Minister’s Office-Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Youth, Employment and People with Disabilities. It has been set up with the aim of improving health and wellbeing of workers and of workplaces. This will be achieved by promoting occupational health and safety(OHS) practices in order to prevent occupational injuries and diseases and ultimately achieve better productivity
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi ni Taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa
mujibu Sheria ya Wakala wa Serikali Namba 30 ya mwaka 1997 ambapo majukumu yake
yameainishwa katika Sheria Ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Namba 5 ya Mwaka
2003. Wakala pamoja na kazi nyingine una dhamana ya kusimamia Usalama na Afya za
Wafanyakazi wanapokuwa kazini.
Ili kuhakikisha kuwa Wakala unatekeleza Majukumu kama yalivyoainishwa katika
sheria tajwa hapo juu, Mtendaji Mkuu anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa
na uwezo wa kujaza nafasi zipatazo Kumi na Sita (16) za Kada tofauti kama ifuatavyo;
1.0 DEREVA II (NAFASI 10)
1.1 SIFA ZA WAOMBAJI
i. Awe na cheti cha kidato cha nne (Form IV)
ii. Awe na leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari.
iii. Awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
iv. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
v. Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II wataanza
kufikiriwa.
1.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
vi. Kufanya usafi wa gari.
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
1.3 MSHAHARA
OSHA 3.1 kwa mwezi.
2.0 MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI (NAFASI 4)
2.1 SIFA ZA WAOMBAJI
i. Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI).
ii. Awe amehitimu mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu katika ngazi ya
Cheti katika mojawapo ya fani ya Masjala kutoka katika vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
2.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutafuta Kumbukumbu, nyaraka na Majalada yanayohitajiwa
ii. Kuthibiti upokeaji na uandikishaji wa Kumbukumbu
iii. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga Kumbukumbu
iv. Kufungua Majalada mapya yanayohitajika.
v. Kuweka Kumbukumbu (barua, nyaraka, n.k) katika Majalada
vi. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makabati na reki (file
racks/cabinet) katika masijala.
vii. Kuthibitisha Machapisho kwa ajili ya Kumbukumbu za ofisi ndani ya
muda uliopangwa
viii. Kutoa elimu ya mara kwa mara kwa Maafisa wanaokiuka utaratibu wa
uhifadhi wa Kumbukumbu.
ix. Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na Msimamizi wake.
2.3 MSHAHARA
OSHA 3.1 kwa mwezi.
3.0 MHASIBU MSAIDIZI (NAFASI 4)
3.1 SIFA ZA WAOMBAJI
i. Awe na Stashahada ya Kawaida ya Uhasibu (Diploma in Accountancy)
kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
ii. Awe na cheti cha ufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher
Standard Govemment Accountancy Examination) unaotolewa na
Chuo cha Utumishi wa Umma.
iii. Awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika fani ya Uhasibu.
3.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupokea na kulipa fedha.
ii. Kutunza Daftari la fedha.
iii. Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki. (Bank Reconcialiation)
iv. Kukagua hati za malipo.
v. Kupitisha malipo kulingana na Kanuni za fedha.
vi. Kusimamia kazi za Wasaidizi wa Hesabu.
vii. Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na Msimamizi wake.
3.3 MSHAHARA
OSHA 4.1 kwa mwezi.
4.0 MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka
Miaka Arobaini na Tano (45)
ii. Waombaji waambatishe Cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) yenye
anwani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini watatu (3) .
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
v. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa
na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU/NECTA).
vi. Watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za
kisheria.
vii. Maombi yatumwe kwa njia ya Posta au kwa mkono kufikishwa Ofisi za
Makao Makuu zilizopo Kinondoni Barabara ya Mahakama.
viii. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29/12/2017.
ix. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa hayatafanyiwa
kazi.
1.5 JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa;
Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi,
S.L.P 519,
DAR ES SALAAM.

NAFASI ZA KAZI OSHA 2018
Reviewed by Unknown
on
10:53:00 PM
Rating: