Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu
waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe
09/10/2015 hadi tarehe 22/10/2015 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo
vya kazi umekamilishwa.
Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana
katika Tangazo hili. Katika orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi
ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada
mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi
kupatikana.
Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika
muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi
wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato
cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya
ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zitatolewa kuanzia tarehe 25
Novemba, 2015 katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira kwa wale ambao
wangependa kuchukua barua zao katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira.
Ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara
nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI 16 NOVEMBA 2015
TANGAZO LA KUITWA KAZINI 16 NOVEMBA 2015
Reviewed by Unknown
on
1:05:00 AM
Rating: