Ref. Na EA.7/96/01/H/56 9 Julai, 2015
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 599 kwa ajili ya Katibu mkuu Wizara ya maliasili na Utalii kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (BASIC TECHNICIAN)– NAFASI 346
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
1.4 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
• Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
• Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
• Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
• Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
• Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
• Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
• Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
• Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao
• Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi
• Kudhibiti wanyamapori waharibifu
• Kudhibiti moto kwenye hifadhi
• Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
1.5 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.6 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
– Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
– Computer Certificate
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
– Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24 Julai, 2015
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo vya kazi.
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (BASIC TECHNICIAN)– NAFASI 346
Reviewed by Unknown
on
12:30:00 AM
Rating: